29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Gonzalo Higuain atangaza kustaafu soka

BUENOS AIRES, ARGENTINA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Juventus, Gonzalo Higuain ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Chelsea kwa mkopo, ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Argentina huku akiwa na miaka 31.

Mara ya mwisho mchezaji huyo kuitumikia timu hiyo ilikuwa mwaka jana kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, lakini alishindwa kuisaidia kufanya vizuri.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akisemwa vibaya na mashabiki wa timu hiyo tangu kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, ambapo alishindwa kuisaidia timu hiyo baada ya kutinga fainali huku akipata nafasi nyingi za wazi lakini alishindwa kuzitumia.

Mwaka 2015 kwenye michuano ya Kombe la Copa America, alikuwa kwenye kiwango cha chini na watu wakazidi kuuliza maswali mengi juu ya kiwango chake wakati wa kuitumikia timu hiyo ya taifa.

Mshambuliaji huyo mara ya mwisho kufunga bao akiwa anaitumikia timu ya taifa Argentina ilikuwa Oktoba 2016, katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, mchezo huo ulikuwa dhidi ya Peru, lakini hakuweza kufunga bao hata moja nchini Urusi kwenye Kombe la Dunia mwaka jana hadi timu hiyo inatolewa katika hatua ya 16 bora.

“Nadhani sasa nimefikia mwisho kuitumikia timu ya taifa, kwa sasa nataka kuyafurahia maisha na familia yangu, kwa sasa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi juu yangu kama nitakuwa kwenye kikosi au sitokuwepo, ukweli ni kwamba muda wangu wa kuachana na timu umefika, sina sababu ya kuendelea.

“Kuna watu wamekuwa wakifurahia kukosoa, lakini ni wagumu kusapoti, hivyo ngoja niwaachie timu na wachezaji ambao wanaaminika kama watafanya vizuri, nawatakia kila la heri,” alisema mchezaji huyo.

Kutokana na kushindwa kuisaidia timu, kocha wa timu hiyo, Lionel Scaloni, anataka kuwatumia Mauro Icardi, Lautaro Martinez, Dario Benedetto na Matias Suarez katika nafasi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles