25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Gondwe afurahishwa na utendaji wa SOS

Na MWANDISHI WETU – DARE S SALAAM

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amezitaka taasisi na asasi nyingine nchini kuiga mfano wa SOS Children Village ambayo imekabidhi mradi wa madarasa 10 yaliyofanyika ukarabati na kuyafanya kuwa madarasa yabatyozungumza kupitia mradi wake wa Tucheze na Tujifunze.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa mradi huo mjini Chanika wilayani Ilala, Gondwe ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge alisema mradi huo ni sehemu muhimu ambayo imesaidia kuboresha mazingira na miundombinu ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Alisema kupitia mradi huo umeisaidia seriali katika juhudi zake za kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunzia na kuboresha elimu kwa shule za msingi, hivyo kusaidia kuinua viwango vya ubora wa ufundishaji wa kuongeza ubora wa elimu 

“Katika Mkoa wa Dar es Salaam, hii itasaidia juhudi za serikali ambapo Rais john Magufuli tayari ameshatoa zaidi ya Sh bilioni 45.8 kwa ajili ya elimu na kuhakikisha watoto wanasoma na kukua kisha kuwasaidia wazazi wao na kwamba, inaweza kuwasaidia wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wao hawakai mtaani, bali anapata fursa ya kusoma,” alisema.

Alisema amepokea madarasa 22 na madarasa mawili ya awali na maktaba ya wanafunzi kusoma lakini katika uzoefu uliopatikana katika ushirikiano wa Serikali na wadau wakiwemo SOS, imesaidia kutoa maelekezo kwamba wale walimu waliopewa mafunzo waendelee kupeana uzoefu katika kata zote walipo.

Gondwe alisema kwamba madarasa hayo yanatakiwa yaendelee kuwa madarasa yanayoongea na wanafunzi waweze kujifunza kwa kuona, akiziomba taasisi na wadau wengine wajitokeze kusaidia kuinua elimu katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuwa kwa juhudi hio za serikali kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bila malipo itasaidia kuondoa kabisa idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika na kwamba itasaidia kuwa na taifa la watu wenye elimu.

Alisema hiyo ni pamoja na kuendelezwa kwa elimu kwa walioikosa (Memkwa) ambapo uongozi wa ngazi ya kata unatkiwa kuhkikisakwamba wale wote wasiopata elimu wanafikiwa na kupata elimu.

Alisema utaratibu kwa ajili ya kuwawezesha wasiopata elimu kupata elimu umeshaandaliwa kila kati kwa hiyo ni wajibu wa maofisa elimu ngai ya kata kuhakikisha wanawafikia wote wanaohitaji kufikiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi wa SOS, Elam Kayange alisema mradi huo wa Cheza na Jifunze, ulinuia kuboresha mazingira na miundombinu kwa kutambua kuwa mazoezi yana mchango mkubwa kwa wanafunzi kujifunza.

Kayange alisema baada ya kukamilisha mradi huo wameukabidhi kwa serikali kw aajili ya kuisimamia na kuiendelea.

Mwenyekiti wa Bodi ya SOS Zanzibar, Nassor Mohamed alisema ujenzi huo umewasaidia watoto wakiwemo waliokosa fursa kupitia Memkwa na kwamba utakuwa na masaada mkubwa kwa siku zijazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles