30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Golden Tulip yafutiwa umiliki wa kiwanja

Lukuvi+PHOTONA RUTH MNKENI, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema imekubaliana na wamiliki wa Hoteli ya kitalii ya Golden Tulip iliyopo Masaki, Dar es Salaam kukifuta rasmi kiwanja namba 2048 ambacho awali walikimiliki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Hassan Mabuye, wamiliki hao wameridhia ombi la Serikali la kufuta umiliki wa kiwanja hicho.

Taarifa hiyo ilisema wamiliki hao walifika ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kueleza lengo lao la kuunga mkono mpango huo wa Serikali, na kwamba wamekubaliana na uamuzi wa matumizi ya eneo hilo lililo jirani na hoteli yao.

“Wamiliki hao wamesema wao ni raia halali wa Tanzania wanaoishi kwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi na kamwe hawawezi kuingia kwenye mvutano na Serikali au kutotii maagizo yake,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa upande wake, Waziri Lukuvi aliwashukuru wamiliki hao kwa kukubaliana na uamuzi wa Serikali na akaongeza kwamba tayari wamefuta rasmi hati iliyotolewa kwao juu ya umiliki wa kiwanja.

Januari mwaka huu, Serikali ililazimika kuvunja uzio wa eneo la kiwanja hicho kilichopo Msasani Peninsula ili kuzuia uendelezaji wake kwa kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya matumizi ya umma.

Umiliki wa kiwanja hicho ulibatilishwa rasmi Februari Mosi, mwaka huu na kurudishwa serikalini baada ya kuonekana kilimilikishwa kinyume cha taratibu za sheria za ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles