22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Gohere Tanzania kuchochea utalii kwa kuwasaidia watalii kupata hoteli

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kampuni ya GOHERE Tanzania imeanzisha huduma ya kutafuta hoteli na vivutio kwa kutumia simu janja ili kuwarahishia watalii na kuhakikisha teknolojia inakua katika sekta ya utalii.

Akizungumzia Oktoba 6, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya S!TE yanayoendelea Mlimani City Mkurugenzi Mkuu na Muanzilishi wa Gohere, Menno Biesiot amesema kufuatia filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imevutia watu wengi zaidi kuja kuwekeza nchini.

Amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini hivyo kwa kutumia huduma hiyo(application) itasaidia mtalii anapokuja nchini kuweka nafasi (booking) ya hotel atakayofikia pia na sehemu atakazotembelea.

“Hii Application ni njia rahisi ya mtalii kutumia pindi anapotaka kuja nchini itamsaidia kujua hoteli zilizopo sehemu anayotaka kwenda lakini pia gharama, hii itasaidia kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa maana amesaidia sana kutangaza utalii wa hii nchi,” amesema Biesiot.

Naye, Meneja Rasmali watu na Utawala wa Kampuni hiyo, Winfrida Msabuni amesema kampuni hiyo imejidhatiti kutoa huduma nchini kwa kuvutia watalii wengi kwani hiyo imekuwa njia rahisi na ya haraka.

“Hii kampuni ipo sehemu mbalimbali duniani na imekuwa ikifanya vizuri, kuanzishwa kwa huduma hii nchini kutasaidia kuzidi kuvutia watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, hivyo nitoe rai kwa watu kuitumia,” amesema Msabuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles