30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Goba, Wazo, wahakikishiwa maji ya uhakika Februari mosi

TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

SERIKALI imewathibitishia wakazi wa Kata ya Goba, Manispaa ya Ubungo na Wazo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam uhakika wa kupata maji safi na salama kuanzia Februari mosi mwaka huu.

Akizungungumza baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alisema Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imepeleka vijana 50 kukamilisha mradi wa usambazaji maji katika maeneo hayo.

Alisema vifaa vyote vimefikishwa katika eneo hilo na vijana wameanza kazi rasmi.

“Kuanzia Ijumaa Februari mosi maji katika maeneo haya yataanza kutoka na kila mwananchi atapata maji safi na salama,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema katika mitaa ya Kinzudi na Kwa Ubarikio iliyopo katika kata hizo wanatarajia kuunganisha wateja wapya 700 na kuongeza mapato ya Dawasa.

“Tunakiri kukosea kwa kuwa hakukuwa na haja ya mradi huo kuchelewa kutokana na kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja, na sasa tumekubaliana kuwekeza nguvu katika mradi mmoja na utakapokamilika tunahamia mwingine,” alisema.

Kwa upande wao, wakazi wa mitaa hiyo wameishukuru Serikali kwa kuwaahidi kupata maji kwani wamekuwa wakiteseka kwa kutumia muda mrefu kutafuta maji.

Mmoja wa wakazi hao, Josephat Nihuka alisema wamechimba mitaro ili wapatiwe huduma hiyo ambapo kwa sasa wanaishukuru Dawasa kuwatua mzigo huo.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa maji katika maeneo haya kwani wananchi wamekuwa wakiilaumu Serikali,” alisema Nihuka.

Naye Waziri Rajab aliitaka Dawasa kuhakikisha inapeleka mafundi na vifaa kwa wakati ili kurahisisha zoezi la usambazaji maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles