24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Giniki: Nikipata nafasi Omlipiki nitaleta Medali nyumbani

GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

MWANARIADHA wa Tanzania, Emmanuel Giniki amezidi kujitangaza kimataifa na kupata mashabiki zaidi kutokana na kufanya vyema kwenye mialiko yake, ambayo amekuwa akialikwa.

Kutokana na umaarufu huo, baadhi ya wadau wamejitokeza, wakitaka kuinunua jezi yake kwa gharama yoyote ile.

Tukio hilo limetokeza nchini Hispania, alipokwenda kushiriki mashindano ya (xxxvi Cross Internacional de Ita’lica) ya 10 km mwaka jana, aliyomaliza nafasi ya tano akitumia wa dakika 31:08, huku wa kwanza akiwa Joshua Cheptegei wa Uganda aliyetumia dakika 30:54.

Nyota ya mwanariadha huyo, inaendelea kung’aa katika mashindano mbalimbali, anayoshiriki yakiwamo ya kitaifa na kimataifa.

Mwanariadha huyo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), pia aliweza kuibuka bingwa wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon, yaliofanyika Februari 16 mwaka huu, mkoani Kilimanjaro.

Katika mashindano hayo ya Kili Marathon, Giniki alimaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:03.34, akifuatiwa na Musa aliyetumia saa 1:03.42, nafasi ya tatu ikienda kwa Joseph Njihia wa Kenya aliyamaliza kwa saa 1:05.13.

Kabla Giniki kushiriki mashindano ya Kili Marathon, alikuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya Majeshi yaliofanyika Februari 24 hadi Machi 8 mwaka huu, katika mbio za km 5000 jijini Dar es Salaam.

Pia kabla ya mbio hizo alifanikiwa kushiriki mashindano ya Sio Silvestre, yaliofantika mwaka jana na kufanikiwa kushika nafasi ya nne, huku (Lageda 35 Corrid De Reis) akishika nafasi ya pili katika mashindano hayo, yaliofanyika Januari mwaka huu, nchini Brazil.

Spotikiki, lilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Giniki ili kujua changamoto, anazopitia pamoja na maandalizi kuelekea mashindano ya Mbio za Nyika, Denmark Machi 30 mwaka huu.

MAANDALIZI YA NYIKA

Giniki amesema asilimia kubwa anamatumaini ya kushiriki na kiufanya vizuri katika mbio za nyika zinazotarajiwa kufanyika Machi 30 mwaka huu nchini Denmark.

“Ninaendelea na maandalizi maana nilikuwa na majeraha kidogo kwenye goti, hivyo ninajipanga kuhakikisha naiwakilisha vyema nchini yangu.

Anasema mashindano hayo yatazidi kumjenda kwa ajili ya kushiriki mashindano mengine ya kimataifa, ambayo yapo mbele yake yakiwamo Olimpiki.

AKIPATA NAFASI KUSHIRIKI OLIMPIKI

Giniki anasema endapo atafanikiwa kushiriki Olimpiki hapo mwakani, itakuwa ni fahari kubwa kwake na atahakikisha anarudi na medali

“Hakuna mwanariadha asiyependa kushirki mashindano hayo makubwa dunaini, ndoto za kila mmoja wetu ni kupiga hatua na kulitangaza taifa lake.

CHANGAMOTO

Giniki anasema changamoto kubwa iliyopo ni kukosa kushiriki baadhi ya mashindano kutokana na kubwana na kazi.

“Kwa walioajiriwa kama mimi inakulazimu kuacha mashindano na kuitumikia kazi, ambayo umeajiriwa hivyo inakufanya kukosa baadhi ya vitu vingi na pengine ungeweza kushinda.

Anasema pia changamoto nyingine ni kukosa ufadhili, ambapo wanariadha wengi wanakuwa hawana vifaa vya mazoezi, hasa raba maalumu za kukimbilia.

“Mara nyingi tunakabiliwa na ukata, ambao unafanya mtu anashindwa kununua raba na matokeo yake anakimbia peki, jambo linalosababisha kupata maradhi mengi, kwani unaweza kukanyaga vitu vyenye ncha kali ambayo vitakuumiza.

TANZANIA TUNAKWAMA WAPI

“Tunafanya maandalizi kwa muda mfupi, labda wiki mbili kwa ajili ya mashindano ya kimataifa, huku wenzetu wakiwa kambini miezi mitatu, hatuwezi kushindana nao hata kidogo, tunahitaji kuandaliwa kwa muda mrefu ili kuweza kushiriki vyema mashindano.

Alieleza  kuwa Tanzania, bado haina mazoea ya kufanya mashindano ya mara kwa mara, ambayo yatamuwezesha mkimbiaji kuzoea na kuboresha viwango.

“Kawaida wanariadha wanatakiwa kupewa mashindano ya mara kwa mara, labda akishiriki leo anatakiwa keshokutwa ashiriki tena, akipumzika wiki moja viungo vinachoka na anashindwa kukimbia tena katika kiwango kile cha awali.

NINI KIFANYIKE

Giniki anasema ili kuitengeneza Tanzania ya wakimbiaji na michezo, lazima vijana waanze kufundishwa wakiwa na  umri mdogo, ili baadae waweze kuwa bora kwa taifa.

“Tunahitaji kuwapika wanariadha tangu wakiwa wadogo, wengi wanavipaji, lakini hawajui watavionyesha wapi, tukifanya hivyo tutavuna medali nyingi kila mashindano.

 â€œNinavyojua kwa kila wiki mwanariada anatakiwa kushiriki mashindano hata mara mbili au tatu, kunamfanya kujiamini na kujua nini anafanya, lakini ikiwa ni hadi mashindano kwa mashindano tutazidi kufeli.

Alieleza kuwa serikali wanatakiwa kutoa vifaa vya michezo hasa jezi na viatu ili kumshawishi mwanariadha kujiamini na kupenda kile anachofanya, wengi wanashindwa kutokana na kukosa vitu muhimu.

%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%%

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles