24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

GIGGY MONEY: SIKUMBUKI WANAUME NILIOTOKA NAO

Gift Stanford ‘Giggy Money’
Gift Stanford ‘Giggy Money’

Na KYALAA SEHEYE,

STAA wa kike Bongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ anayetingisha kwa ishu kibao mjini, amefunguka kuwa anapenda maisha yake na hajali watu wanavyomchukulia tofauti.

Akipiga stori na Swaggaz, Giggy ambaye ni mtangazaji wa Radio Choice FM, Video Vixen na msanii wa Bongo Fleva, amesema skendo zake ndizo zinazompaisha na haoni tabu hata kidogo kusemwa au kuandikwa kuhusiana nazo.

“Watu wananiita majina mengi, shauri yao. Sijali. Mimi naendelea na maisha na napiga pesa… ninachofanya ni idea yangu ya kutengeneza pesa, ndiyo maisha niliyochagua,” anasema.

Mwandishi wa Swaggaz amezungumza naye mengi. Fuatilia mahojiano yetu hapa chini.

MY STYLE: Kwanini picha zako nyingi unazotupia Insta ni za mitego?

GIGGY MONEY: Picha za mitego Insta ni idea yangu ya kupiga hela… ni entertainment, napenda kuwa vile, ni maisha yangu, nipo free nayo. Sioni tatizo na naona nipo sawa. Sifanyi labda ili mtu anifanyie chochote, hapana. Napenda kuwa vile. Ni maisha niliyoyachagua.

MY STYLE: Unaye boyfriend? Kama huna, sifa za boyfriend wako ni zipi? Unapenda mwanaume wa aina gani?

GIGGY MONEY: Yeah! I have a boyfriend lakini sidhani kama mapenzi yanatangazwa. Kwa kawaida hujitangaza yenyewe. Napenda mwanaume mstaraabu, anayejielewa na mwenye mapenzi ya kweli. Anayejali na kunithamini, sijali sana awe na pesa au asiwe nazo ni sawa.

MY STYLE: Nini kinaendelea kati yako na Gadner G. Habash?

GIGGY MONEY: Gardner ni rafiki yangu wa karibu sana, sana, sana kuliko unavyofikiria. Sipendi kuongea sana kuhusu hii ishu, kwa sababu napenda watu wakikasirika, hata kama mimi nikitembea na Garder hakuna mtu inamuhusu Tanzania nzima.

MY STYLE: Kwanini uhusiano wako na Gardner ulivuma kipindi kile alipokuwa hayupo sawa na mtalaka wake Jide?

GIGGY MONEY: Kuhusu competition ya kunicompete na Jide ilikuwa ni wao, kwa sababu alitoka kuachana na Jaydee halafu na Tanzania kama unavyoijua wananichukuliaga kama zoazoa, nikaona sio mbaya nikimzoa na huyo Gardner wao.

Kwahiyo inawezekana nikawa nimetembea naye au sijatembea naye, hiyo ni kazi yangu mimi. Kuachana kwake na Jaydee havinihusu, wao ni watu wazima. Mpaka wamefikia kuachana wameamua.

MY STYLE: Mwanamuziki gani kwenye game anakutisha?

GIGGY MONEY: Hakuna mwanamuziki anayenitisha, muziki siyo mashindano. Naamini muziki ni ushirikiano, wanaofanya mashindano wanakosea.

MY STYLE: Ukipewa bilioni moja sasa hivi, utaifanyia nini?

GIGGY MONEY: Nikipewa pesa hiyo nitaiingiza kwenye biashara, hata hivyo bilioni moja siyo pesa nyingi, always hakuna pesa inayotosha.

MY STYLE: Kwanini wasanii wengi wa kike wanajihusisha na skendo za mapenzi?

GIGGY MONEY: Skendo zinawafanya wasanii wawe juu, ila inategemea unahusishwa na nani na ni skendo gani. Siyo kila msichana anayehusishwa na skendo anakuwa juu, siyo watu wa ovyo ovyo tu. Inategemea ni nani, anafanya nini na nani. Siyo vipenzipenzi tu, vijitujitu tu.

MY STYLE: Unakumbuka idadi ya wanaume uliotoka nao kimapenzi?

GIGGY MONEY: Kwakweli sikumbuki, labda kwa mastaa naweza kukuambia. Nimetoka na Abdukiba, Ali Kiba (hawa ni ndugu wa damu), Hemed Phd, Rich Mavoko, Harmonize na Casto Dickson. Huyu nilitamani hata kuzaa naye, wanawake wa mjini waliharibu penzi letu.

MY STYLE: Umewahi kuvuta bangi? Mara ngapi?

GIGGY MONEY: Hata kama nimeshawahi kuvuta, lakini kwa sasa hivi haina manufaa katika maisha yangu, hainiongezei chochote, hainisaidii chochote. Sanasana nakuwa siyo mimi, huwa najiamini nikiwa mzima kama hivi ninavyoongea na wewe. Ndiyo maana nikaamua kutulia, niendelee na maisha yangu. Nilitumia wakati huo, sasa nimeacha.

MY STYLE: Jambo gani linakukera zaidi kwenye uhusiano wa kimapenzi?

GIGGY MONEY: Aisee sipendi uongo, always uongo. Sipendi kabisa kudanganywa, sipendi mtu anidharau. Napenda kuheshimiwa.

MY STYLE: Ukipata nafasi ya kukutana na Rais Magufuli sasa hivi, utamweleza changamoto gani zilizopo mitaani?

GIGGY MONEY: Nitakachoweza kumwambia mheshimiwa John Pombe Magufuli, nitamwambia daah! Mtaani pamechafuka, hali imekuwa mbaya, pesa hakuna. Hapa kazi tu, kama alivyosema mwenyewe.

MY STYLE: Ukipata nafasi ya kufanya colabo na msanii wa kimataifa, utamchagua nani?

GIGGY MONEY: Mtu ninayetamani kufanya naye kolabo leo, kesho hata sasa hivi,  sidhani kama bado yupo hai… ni Monique Séka au kwa wasanii wa kizazi cha sasa kwa nje ni  Selebobo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles