30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

GHASIA ATAKA TOZO ZA HUDUMA ZIACHIWE HALMASHAURI

Hadija Omary, Mtwara

Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia ameiomba serikali kusitisha mpango wake wa kutaka kukusanya tozo ya huduma kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na badala yake waziache kwenye halmashauri husika.

Ghasia ametoa ombi hilo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana katika ghafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia Mtwara iliyofanyika katika Viwanja vya Bandari mjini hapa.

Ombi la Ghasia limekuja baada ya kupokea barua kutoka TRA kuwa ifikapo Juni mwaka huu tozo hiyo ambayo ilikuwa inatozwa na halmashauri husika itatozwa na mamlaka hiyo.

Amesema katika nchi zote zinazoendelea haijawahi kutokea tozo ya huduma ya halmashauri ikakusanywa na serikali kuu, na hata maeneo mengi  yenye miradi ya gesi wananchi wa maeneo husika wanapata manufaa ya gesi hiyo lengo kubwa likiwa ni kuleta utulivu.

“Ukienda Msimbati wakati wa uchimbaji wanapojaribisha visima vyao usiku mji wao unawaka umeme tu sasa wanapata nini katika ile kama umeme tutapata nchi nzima, kama gesi tutapata nchi nzima nikuombe Waziri Mkuu tozo ya huduma  mtuachie,” amesema ghasia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles