25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

GEREJI DAR ZAFURIKA MAGARI ‘MIKWECHE’

Na ASHA BANI, Dar es Salaam

BAADA ya Serikali kutangaza kufuta ada ya mwaka ya leseni ya magari na badala yake ada hiyo ilipwe mara moja tu gari linaposajiliwa, magari yafurika gereji kwa matengenezo   yaweze kuingia barabarani   mwaka wa fedha 2017-2018 ukianza.

MTANZANIA limeshuhudia na kuzungumza na baadhi ya mafundi wa gereji mbalimbali za  Dar es Salaam juzi na jana, walioeleza maoni yao kuhusu msongamano huo.

Akizungumzia hilo fundi Mohamed Omary wa gereji ya Magomeni Mapipa alisema   walikuwa wamekaa bila ya kazi lakini  kwa sasa wameelemewa.

Alisema wanapokea magari mabovu ambayo anaamini yalikuwa yameegeshwa  siku nyingi kutokana na ubovu huo na kushindwa kulipia ada ya mwaka lakini kwa sasa yataingia barabarani.

Ramadhan Juma  wa Yombo Vituka alisema katika kituo chake cha kuziba pancha matairi, anapokea matairi mengi ya kuweka viraka na mengine kuyajaza upepo  na akiwauliza wateja wake wengi wanamjibu yalikuwa hayatumiki.

“Kuna mteja mmoja alikuja hapa na nilipozungumza naye alinambia gari lilikuwa na deni limefika hadi milioni tatu lakini kutokana na serikali kufuta deni hilo  hana budi kutengeneza na kuliingiza barabarani   kuendelea na shughuli zake ,’’alisema Jumja.

Nassoro Yassin wa Buguruni Malapa naye amelieleza gazeti hili kuwa wanapokea magari mengi  kwa sasa  tofauti na ilivyokuwa awali.

“Na tukitupia macho kwenye leseni  tunaona imekwisha kitambo ndipo tunagundua kuwa kumbe tangazo la kuondoa ada imewaibua wengi,’’ alisema Yassin.

Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wa magari wameingiwa na wasiwasi kwamba kutakuwa na mrundikano wa magari barabarani ambayo yatachangia kuongezeka foleni jijini.

Hivi karibuni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philipo Mpango, wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017-2018  bungeni Dodoma, alisema  baada ya kufutwa kwa ada hiyo itaendelea kulipwa kupitia ushuru wa petrol ina dizeli   na mafuta ya taa.

Alisema wakati wa usajili  mara ya kwanza ongezeko litakuwa ni   Sh 50,000 kwa gari yenye ujazo wa  wa injini 501 -1500 CC yaani  kutoka kiwango cha sasa cha Sh 150,000 ikiwa ni ongezeko la Sh 50,000.

Gari lenye ujazo  wa injini ya 2501 cc na zaidi kutoka kiwango cha sasa cha Sh 250,000 hadi Sh 300,000 kwani ongezeko la Sh 50,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles