29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Geita Gold FC mambo safi, basi jipya lawasili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

HATIMAYE changamoto ya usafiri kwa timu ya Geita Gold FC. imetatuliwa baada ya basi jipya la timu hiyo lililoagizwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), kuwasili.

Hatua hiyo imetajwa kuwa chachu kuelekea mchezo wa kesho kati ya Geita Gold na Yanga unaotarajiwa kupigwa jijini Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa mechi za mzunguko wa Ligi Kuu Bara.

Basi hilo limewasili Alhamisi mjini Geita baada GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara kumega sehemu ya udhamini huo kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri kwa timu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi hayo, Meneja Mwandamizi anayeshughulikia maendeleo ya jamii, Gilbert Mworia amesema kukabidhiwa kwa basi hilo ni anaamini itakuwa chachu ya ushindi wa timu hiyo kuelekea mchezo kati yake na Yanga.

Amesema GGML imetoa basi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa uwajibikaji kwa jamii – CSR.
Ameongeza kuwa basi hilo linatarajiwa kukabidhiwa kwa uongozi wa timu katika hafla itakayofanyika wiki ijayo.
“Basi hili litasaidia maendeleo ya timu yetu katika safari zake pindi wanaposhiriki michezo ya ligi kuu kuzunguka mikoa mbalimbali na hata nje ya nchi pale itakapolazimika,” amesema.

Amesema mchakato wa kununua basi hilo ulichukua muda mrefu lakini anaushukuru uongozi wa timu na wadau wake kuwa wavumilivu.

“Sasa wana furaha… watembee kifua mbele kwani pia watapata muda wa kwenda kushiriki michuano mbalimbali bila kikwazo cha usafiri.
Amesema ufadhili wa GGML kwa timu hiyo ni wa aina tatu ambao ni pamoja na suala la usafiri ww timu.

“Pili ni kwenye malazi na chakula kwa ajili ya timu kwa muda wote wa mashindano. Tatu miundombinu kama ilivyo sasa tupo kwenye ujenzi wa Uwanja mpya wa kisasa hapa Magogo,” amesema.

Amesema ufadhili mwingine ni wa masuala ya vifaa vya michezo ikiwamo jezi, bukta, viatu na vifaa vingine.

Amesema katika ujenzi ww uwanja huo ambao ulisimama kwa muda, GGML imejipanga kuendeleza ujenzi kwa nguvu zote ili timu ipate mazingira mazuri ya michezo.

Aidha, ameahidi kwamba GGML itaendelea kufadhili timu hiyo na hata kushiriki katika michezo ya ndani na nje ili kuchochea maendeleo ya michezo nchini hasa ikizingatiwa michezo ni ajira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles