27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Gazidis afunguka kuhusu Wenger

ivan-gazidisLONDON, ENGLAND

MKURUGENZI Mkuu wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, akieleza kuwa klabu hiyo inajiandaa na maisha bila ya kocha huyo ambaye mkataba wake unatarajia kumalizika mwakani mwishoni mwa msimu.

Gazidis alitoa kauli hiyo licha ya kocha huyo kuthibitisha kutoongeza mkataba mpya wa kuifundisha timu hiyo baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika.

Kiongozi huyo pia alisisitiza kuwa klabu hiyo si mali ya Wenger na kuongeza kuwa chochote kinaweza kutokea mwishoni mwa msimu.

Hata hivyo, Arsenal hadi sasa imepoteza mchezo mmoja katika michezo saba tangu msimu uanze na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu England ambao unaongozwa na Manchester City.

Zaidi ni kwamba, Gazidis alieleza kuwa klabu hiyo haina wasiwasi kuhusu maisha ya baadaye ya kocha huyo.
“Wenger yupo sahihi na klabu pia ipo sahihi, kila siku tupo makini kufanya uamuzi wenye manufaa na tija ili kuhakikisha tunapata maendeleo.

“Hata hivyo, bado tupo katika mazungumzo na kocha huyo ndipo tuendelee na utaratibu mwingine,” alisema Gazidis.

Gazidis aliongeza kuwa wanatakiwa kufikia makubaliano na kocha huyo kabla ya kufanya uamuzi wowote kwa kuwa Wenger ameiweka klabu hiyo sehemu sahihi katika soka.

Wenger pia anatakiwa na Chama cha Soka cha England ili kuifundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo baada ya Sam Allardyce, kujiuzulu mwezi uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles