27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

GARI LA WAGONJWA LAPATA AJALI LIKITOROSHWA USIKU

Na DERICK MILTON-SIMIYU

SIKU chache baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kupiga marufuku magari ya wagonjwa (ambulance) kubeba kitu chochote zaidi ya mgonjwa, gari la wagonjwa la Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu limepata ajali huku likiwa limebeba matairi 9 chakavu.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya habari kutoka ofisi ya Mkuu wa  Wilaya ya Itilima zilieleza kuwa gari hilo lenye namba za usajili STK 6646 linadaiwa kupata ajali hiyo majira ya saa 10 usiku wa kuamkia jana katika eneo la Daraja la Mto Bariadi, katikati ya Mji wa Bariadi baada ya kutoroshwa kwenye maegesho ya Serikali, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijafahamika.

Taarifa hizo zilieleza kuwa wakati gari hilo linapata ajali halikuwa na mgonjwa yeyote, ambapo dereva aliyefahamika kwa jina la Ndekeja Makwenu amelezwa katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu akipatiwa matibabu kutokana na marejaha mbalimbali aliyopata.

Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya ya Itilima, Paul Nyalaja alisema kuwa gari hilo ni moja ya magari manne yaliyopelekwa mkoani Mwanza siku ya jumapili wiki iliyopita kwa ajili ya matengenezo.

Nyalaja alisema baada ya matengenezo hayo gari hilo ndilo lilibeba matari yote ya magari manne, ambayo yalikuwa chakavu kwa ajili ya kuyarejesha ofisi za usafirishaji za halmashauri hiyo kama taratibu za manunuzi zinavyoelekeza.

“Gari lilifika Bariadi siku ya jumatu usiku na kuegeshwa katika kituo cha Afya Muungano kilichopo Mjini Bariadi, katika mazingira ya kutatanisha muda wa saa 10 usiku, gari liliondolewa kwenye kituo hicho cha Afya kuelekea kusikojulikana,” alisema Nyalaja.Aidha, alisema walishangaa kukuta gari hilo limepata ajali, likiwa na limebeba matari hayo huku likionekana limegonga tela la trekta lilikuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika.

Kaimu Mkurugenzi huyo alieleza uchunguzi wa kubaini chanzo cha ajali na sababu za gari hilo kuondolewa kwenye maegesho ya magari ya Serikali nyakati za usiku unaendelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya, Benson Kilangi alisema hakuna kifo kilichotokea kwenye ajali hiyo.

Kilangi alisema ameagiza kukamatwa kwa Afisa Usafirishaji wa Halmashauri, Oswini Mlelwa ili asaidie uchunguzi.

“Mbali na kukamatwa kwa afisa huyo, nimemwagiza Mkurugenzi achukue hatua za kinidhamu kwa wahusika wote lakini pia nimeagiza jeshi la polisi kumweka chini ya ulinzi dereva wa gari hilo ambaye yuko hospitali akipatiwa matibabu,” alisema Kilangi.

Alisema magari ya Serikali yana taratibu zake namna yanavyoweza kufanya kazi hata kama kuna dharura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles