25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Gambo aongoza mazishi ya mwanahabari Mbonea

Janeth Mushi -Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ameongoza mamia ya wananchi, wadau wa habari, ndugu na jamaa katika mazishi ya Eliya Mbonea ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, ambayo inachapisha magazeti ya MTANZANIA, Rai, Bingwa, Dimba na The African.

Mwanahabari huyo alifariki dunia Dar es Salaam Aprili 6 mwaka huu, wakati akiendelea kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Tangu Oktoba mwaka jana, Mbonea alikuwa akitibiwa Hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), kwa nyakati tofauti na baadaye kuhamishiwa MNH.

Mazishi ya Mbonea yalifanyika makaburi ya Njiro jijini Arusha jana na yalihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu na viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa.

Akizungumza na MTANZANIA, msemaji wa familia, Wilfred Hume alisema Mbonea alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuishiwa damu.

“Wakati huo alianza kuumwa nimonia akapatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC akapona ila baadae akaumwa tena homa ya manjano akafanyiwa operasheni, baada ya hapo miguu ikaanza kuvimba.

“Tukamrudisha tena KCMC wakaja kugundua kuwa alikuwa na uvimbe tumboni, wakamtibu huo uvimbe ikawa hautoki na damu ikawa inamuishia, wakasema tumpeleke Muhimbili,” alisema Hume.

Alisema kuwa Mbonea alivyofika Muhimbili alitibiwa kwa wiki tatu hadi umauti ulipomkuta.

Akiongoza ibada ya maziko, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK), Dk. Stanley Hotay, alisema katika kipindi cha miezi sita ya mwisho, imani ya Mbonea ilionekana kuongezeka  na kuwa aliishi maisha ya ukamilifu siku zake za mwisho.

Alisema Mbonea pia alikuwa dereva wake kwa wakati mwingine na kuwa kanisa linaumia kutokana na upendo wake kwa wengine.

“Tunaumia kwa sababu upendo wake ni mgumu sana kusahau, ni mtu ukimwagiza jambo anafanya na kuzidisha, msikivu, amenitambulisha kwenu wanahabari, igeni mazuri yake, tabia ya kuthubutu kusema, nawaomba maadili yenu yawe mema, kama kuna namna ya kumuenzi ni kujifunza kupitia mazuri yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles