26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Gama Gaming Limited yazindua mchezo wa Bahati SMS kuleta burudani kwa watumiaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mazingira ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania yamebadilika kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 kupitia mchezo wa pool betting juu ya ushindani wa Simba na Yanga hadi kudhibitiwa mwaka 1967 kupitia sheria ya pools na bahati nasibu.

Meneja wa Tehama wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Kabora Mboya, akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa mchezo wa bahati nasibu wa Kampuni ya Gama, Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Wilfred Magotti.

Aidha, mabadiliko hayo yanaenda sambamba na kukua kwa teknolojiaambayo imekuwa ikichukua sehemu ya ukuaji wake na maslahi ya wachezaji.

Hata hivyo, bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania imekuwa muhimu na katika kuweka kanuni na sera kusaidia ukuaji wa sekta hii.

Hivi karibuni iliripoti juu ya ukuaji wa asilimia sita (6%) wa mapato kutoka kwa mapato ya mwaka jana ya Sh bilioni 132.

Gama Gaming Limited ni kampuni ya michezo ya kubahatisha ambayo hivi karibuni imepewa leseni na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania(GBT) kuendesha bahati nasibu ya SMS chini ya leseni SL000000005.

GGL inazindua jukwaa lake la kwanza la Mchezo wa SMS liitwalo BAHATI, ambalo litatoa uzoefu mzuri wa michezo ya kubahatisha ili kukidhi haja ya Watanzania kwa michezo mbalimbali ya kucheza kwenye USSD kupitia Mobile Money Wallets na baadaye kwenye majukwaa mengine.

Mkurugenzi wa GGL, Wilfred Magoti katika taarifa yake aliyoitoa leo Desemba 13, 2022 ameeleza kuwa kwa kuanza watashirikiana na mitandao ya simu za mkononi ya Vodacom, Tigo na baadaye kuongeza Airtel na Halotel kama washirika wakati mchezo ukiendelea na kukua.

“Nia yetu ya kuingia sokoni ilikuwa kuleta michezo na burudani mbalimbali ambazo zilihitajika sana. Hatuwezi kusubiri kuwaonyesha watazamaji na wachezaji wetu kile tunachowawekea katika uuzaji wetu, michezo yetu, shughuli zetu za kijamii na burudani tuliyo nayo.

“Mchezo utakuwa na droo 3 katika saizi na viwango tofauti kulingana na mtu/mchezaji, ambazo ni; Dhahabu Sh 1,000, Almasi 2,000 na Tanzanite Sh 5,000 kwa kila mchezo au tiketi.

“Aidha, kla tiketi ya kucheza ina nafasi kadhaa za kushinda mwanzoni kila tiketi ina nafasi mbili za kushinda wakati wa jackpot ya papo hapo na jackpot ya kila wiki, jackpot zingine zitaongezwa kadiri mchezo unavyoendelea na kuongeza nafasi zaidi kwa kila uchezaji wa tiketi. Kila droo ina uwezekano mkubwa wa kushinda na bei zinazovutia,” amesema Magoti.

Akizungumzia upande wa zawadi, Mtetemela amesema kuwa zawadi za dhahabu ni kati ya Sh 2,000 hadi 200,000, Almasi 5,000 hadi 500,000 na Tanzanite kutoka 10,000 hadi 1,000,000 kwa zawadi za papo hapo. Zawadi ya kila wiki ya jackpot itatangazwa kila wiki na washindi kutangazwa wakati wa onyesho la jackpot litakalofanyika kila wiki.

“Kwa sasa bado hatujatoa programu nyingine zilizopo katika Bahati na namna ya kujiunga ikiwa ni pamoja na tovuti na utumiaji program kwa wiki zijazo, ambapo hii itarahisisha kuelewa kwa watumiaji wetu.

“Hata hivyo, kwa kuzingatia umri, sheria na kanuni zilizowekwa za michezo ya kubahatisha, tungependa kuendeleza uchezaji unaowajibika katika mfumo wetu wote. Kwa mtumiaji yeyote atakayetumia vibaya au kwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa atapigwa marufuku kushiriki katika bahati nasibu yoyote ya mchezo wa BAHATI ulio chini ya Gama Gaming,” amesema Magoti na kuongeza kuwa:

“Kama sehemu ya wajibu wetu wa kijamii tumepanga kuwa mwanachama hai katika jamii yetu na tutashiriki katika nguzo tatu ambazo tumeweka mkazo katika marekebisho ya Elimu, Maendeleo ya Jamii na Huduma ya Afya. Kila nguzo itafunguliwa na kuzinduliwa tunapoendelea. Wateja wetu ni sehemu ya maisha yetu pamoja na sisi na mipango iliyopangwa pia inalenga kuwa sehemu ya mipango yao,” amesema Magoti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles