22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

GADIEL: Wachezaji Simba tunadeni kubwa

 ZAINAB IDDY -DAR ES SALAAM 

BEKI wa kushoto wa kikosi cha Simba, Gadiel Michael, amesema kuwa, wachezaji wa timu hiyo wana deni kubwa la kulipa kwa mashabiki wa klabu hiyo, kutokana na kutimiziwa mahitaji yote muhimu kwa wakati na waajiri wao. 

Gadiel alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na mashabiki wa soka kupitia mtandao rasmi wa kijamii wa klabu hiyo. Gadiel alisema yeye akiwa mchezaji amekuwa akijiona ana deni kubwa awapo uwanjani na kumfanya kujituma ili kuipa mafanikio timu yake hiyo kutokana na mwajiri wao kutimiza mahitaji yao kwa wakati muafaka. 

“Baada ya miaka 10, Simba itakuwa klabu kubwa Afrika kutokana na mipango mingi mizuri inayoweka na viongozi wake chini ya mwekezaji Mohamed Dewij . 

“Tunalipwa fedha na stahiki zetu nyingine kwa wakati huku tukiwa na mazingira rafiki ya kuishi na kufanya kazi, kutokana na hili tunadeni kubwa kwa mashabiki na viongozi ambao wanafanya yote hayo ili kuhakikisha Simba inapata matokeo mazuri kwenye mechi zake za kitaifa na kimataifa,”alisema. 

 Kuhusu ushindani wa namba katika kikosi cha Wekundu hao alisema, hana shaka kwa kuwa bado yupo katika kiwango bora, hivyo anaamini wakati ukifika atakuwa na nafasi ya kudumu. “Nina uhakika nipo katika kiwango kizuri kwa sababu ingekuwa kinyume nisingeweza kuitwa Stars na kupata nafasi , kocha ndiye mwenye uamuzi wa nani ampe nafasi na kwa wakati gani, lakini pia anapopata nafasi mwenzangu bado ni jambo zuri kwani wote tunahitaji mafanikio ya timu,”alisema. 

Gadiel alijiunga na Simba msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga ambayo mkataba wake ulifikia ukomo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles