24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

G7 WAKATAA KUIWEKEA URUSI VIKWAZO

ROMA, ITALIA


MATAIFA saba tajiri yaliyoendelea kiviwanda, maarufu kama G7, yamekataa ombi la Uingereza la kuiwekea Urusi vikwazo baada ya shambulizi baya la kemikali linaloaminika kuendeshwa na mshirika wa Urusi, Syria.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, ilisema kundi la G7 halikuwa na nia ya kuibana Urusi badala yake lilitaka kuwapo mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, kwa sasa anafunga safari kwenda Moscow, Urusi kwa mazungumzo.

Siku ya Jumanne, Vladimir Putin aliutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi huru kuhusu shambulizi la kemikali katika mji unaodhibitiwa na waasi kwenye mji wa Khan Sheikhoun lililowaua watu 89.

Alisema pia amesikia kuwa mashambulizi bandia yanaandaliwa ili kuitupia lawama Serikali ya Syria.

Syria ilikana kufanya shambulizi hilo, lakini Marekani ilijibu kwa kufyatua makombora kwenda kambi ya wanaanga nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Angelino Alfano, ambaye aliandaa mkutano wa G7 katika mji wa Lucca, alisema kuwa mawaziri  walitaka kuzungumza na Urusi kuitaka imshinikize Rais Assad badala ya kuisukuma Urusi hadi kwenye ukuta.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles