RAPA mahiri kutoka kundi la Weusi lenye maskani yake mkoani Arusha, George Mdemu ‘G Nako’, amesema
upendo, umoja, kutodharau na kufanyia kazi ushauri wa mashabiki wao ndiyo misingi inayoliwezesha kundi hilo lisivunjike kama makundi mengine yaliyowahi kuwika kwa muda mfupi kabla ya kusambaratika.
“Sababu hizo tuliziweka kwa pamoja wakati tulipoanzisha kundi letu hilo ambalo kwa sasa ni kampuni.
“Makundi mengi yanasahau kwamba nidhamu ni kitu muhimu katika kila kazi, wengi wao hujitazama binafsi husahau mafanikio ya kundi, huja kwa kuzingatia misingi hiyo tunayotumia sisi na kujikana mwenyewe kwamba ni zaidi ya wenzako,” alisema G Nako na kuongeza:
“Pia sisi tuna kitu kimoja tunakiita heshima kwa mdogo na mkubwa ndiyo maana hatukatai ushari wa yeyote hata ukiwa wa kutuponda tunafanyia kazi ili tukitoka awamu nyingine yule aliyetuponda awe mshabiki wetu, hatupunguzi
mashabiki bali tunaongeza,” anasema G Nako