Future Destin atoa somo kwenye ‘BA OLOBELA’

0
389

BRISBANE, AUSTRALIA

MSANII wa kizazi kipya mwenye makazi yake, Brisbane nchini Australia, Future Destin Fidel a.k.a Future Destin, amewataka vijana kuwaheshimu wazazi wao kupitia wimbo wake mpya, BA OLOBELA.

Future mwenye asili ya Kongo (DRC), ameiambia mtanzania.co.tz kuwa ngoma yake BA OLOBELA imewaongelea watoto ambao hawataki kupokea ushauri mzuri.

“Wimbo una ongelea jinsi watoto hawasikii ushauri, wenye kudharau wazazi na kusema uongo, video nimeiachia jana kwenye chaneli yangu ya YouTube (Future Destin) hivyo mashabiki wanaweza kuitafuta BA OLOBELA na kuitazama,” amesema Destin.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here