23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Fursa za ajira kwa mtandao kuwafi kia waombaji wengi

Lugendo Khalfan - Cheti (1)NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

AJIRA ni kitu muhimu kwenye maisha ya binadamu kwa kuwa baadhi yao uwamini kwamba ndio chanzo cha kumudu gharama na mahitaji katika maisha.

Umuhimu huo ndio sababu ya kuwapo kwa baadhi ya wanafunzi walio kwenye  viwango mbalimbali  vya elimu nchini wanao amini ajira ndio itawafanya kufikia malengo yao endapo watasoma kwa bidii.

Hivyo baada ya kuhitimu elimu yao wanafunzi hao hutumia njia mbalimbali ili kutafuta kazi kwa kuwa wapo ambao kazi hiyo ufanywa na ndugu zao na wengine wakitumia tovuti pamoja na njia nyingine tofauti.

Hata hivyo si wengi kati yao wanaotumia njia hiyo ya tovuti kwani  inadaiwa kuwa ni mpya kwao hivyo kuwafanya kupoteza fursa ya wao kupata ajira zinazotolewa kwa njia hiyo.

Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Jamii Dk. Benson Bana anatoa wito kwa Serikali kuanzisha kituo taifa kitacho toa fursa ya ajira kwa njia ya tovuti ambayo itakuwa ikihusisha taasisi na mashirika ya kiserikali ili kuepuka utapeli unaoendelea.

Anasema kwa kawaida kwenye kutafuta ajira taasisi na mashirika huwa zinatumia njia nyingi na kudai kwamba kwa nchi za Ulaya aina hiyo uitwa ‘job center’ ambapo mtu utembelea kwenye hizo tovuti ilikuona aina ya kazi na vigezo vyake.

“Watu wengi wanaweza kutengeneza mitandao ili kusaidia jambo hilo ambapo kwa upande wa serikali,Sekretarieti ya kazi na ajira wanayo tovuti ya aina hiyo,”alisema .

Akizungumzia tovuti zinazolipisha watu fedha kwamba ni kufanya hivyo ni wizi na kudai kwamba si wote wanaomiliki tovuti hizo wanatabia hiyo kwa kuwa zipo ambao zimekubalika na serikali pamoja na jamii.

“Zipo taasisi zinazokubalika ambazo zenyewe wanapo tafuta waajiliwa zinaomba zitafutiwe kwa kutumia tovuti hizo lakini ili iweze kuaminika ni jambo la busara kujenga kampuni ambayo yenyewe itakuwa wazi.

“Hiyo itakuwa sawasawa kwa kuwa mwenye kampuni naye atakuwa akilipa kodi na kusajiliwa pamoja na kuwa na vigezo vya kuweza kufanya jambo hilo kitaifa vya kuwa kiungo kati ya watafuta kazi na waajili,”anasema.

Anasema kwa kufanya hivyo hapata kuwa na utapeli wa aina yeyote ingawa njia hiyo kwa wanafunzi ni mpya kwao na kudai kwamba mahali anapofanyia kazi (UDSM) ni nadra kusikia wakiitaja njia hiyo ya mawasiliano kwaajili ya kutafuta kazi.

Anasema kwa sasa makampuni binafsi ni nadra kutumia njia hiyo kwa kuwa wengi wao wanatumia ndugu na jamaa zao kutoa nafasi za ajira pamoja na tabia ya kupeana kazi kindugu na kijamaa.

“Mashirika ya Umma ndio mara kadhaa ufanya hivyo lakini hizi kampuni nyingi za mtaani ni wale wale wanaotumia ndugu zao na kubebana.

“Kutokana na jambo hilo Serikali yetu hichangamke, Wizara ya kazi na ajira pamoja na Ofisi ya Rais Menejiment Utumishi wa Umma kwa kupitia Sekretarieti wangeweza kufanya kazi hiyo ya kuwa daraja kwa waajili wanapotafuta watu ili kudhibiti watu wasio kuwa waadilifu katika hilo ambao wamekuwa wakifanya  utapeli,”anasema.

Anasema kazi za kuunganisha waajili na waajiliwa ni vyema zikafanywa na taasisi au makupuni yanayojulikana na Serikali ambayo yamejisajili ili kuondoa hali ya sintofahamu.

Kwa upande wake  muhimtimu wa Shahada ya (Logistic and transport Management) katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), Sarehe Kambona (32)  anasema kuwa mitahala haijawaanda inawafanya wakae kishule shule hivyo inawafanya wasiwe tayari.

Anasema kwamba jambo hilo ni jipya kwa wanafunzi wanohitimu elimu ya vyuo vikuu kwa kuwa wanapokuwa vyuoni hawajiusishi na matumizi ya mtandao hadi wanapokutana na changamoto ya ajira.

“Hata kama ukitumia utumia muda mwingi kusubiri hali ambayo inasababisha kukata tama ya kupata ajira na wengine kuamua ni bora kuendelea kushikwa mkono na ndugu au jamaa zao”anasema.

Naye Meneja Masoko wa tovuti inayounganisha waajiliwa na watoa  ajira,  Brigheter Monday, Lugendo Khalfan    anatoa wito kwa wasomi wanaomaliza elimu yao ya vyuo vikuu na wengine kutoka kweye vyuo vya kawaida kutumia tovuti hiyo kwaajili ya kuwaunganisha na taasis, Mashirika pamoja na kampuni zinazotoa nafasai ya ajira.

Khalfan anasema kuwa kwa kutumia njia ya tovuti kutafuta nafasi ya ajira wasomi wanaweza kupunguza hali ya kuamini kwamba ni lazima kuwapo kwa ndugu au jamaa ili kufanikisha kupata nafasi za kazi nchini.

“Kampuni yetu imesajiliwa na tunafahamika na Serikali ambapo mwaka huu tumepata tuzo ya cheti cha washindi wa pili  katika matumizi ya teknolojia habari na mawasiliano (ICT) ambacho tulikabidhiwa na Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania (Tan Trade) kwenye maonesho ya sabasaba.

“Wapo wanaoamini kwamba ili kupata kazi ni lazima ushikwe mkono na ndugu au jamaa anayekufahamu ambapo jambo hilo sikweli, kwa kuwa sisi tunaweza kuwaunganisha na kupata kazi bila ya kujuana na yeyote zaidi kama umetimiza vigezo vya wahusika,”anasema.

Anasema kwamba kuperuzi tovuti yao  ni bure   ambapo kwa mwezi inwaunganisha watu zaidi ya 3000 wanaotafuta ajira kwenye jumla ya mashirika, pamoja na taasisi za kiserikali na binafsi   zaidi ya 4000 ambayo utoa nafasi mbalimbali kwa wahitimu hao.

Pia Khalfani anadai kwamba tovuto yao  imefanikiwa kupanua huduma zake  kwenye nchi mbalimbali Afrika zikiwamo zinazopatikana Afrika Mashariki  kasoro nchi ya Burundi ambapo kwingine ni Nigeria pamoja na Ghana.

“Kuhusu ngazi ya elimu ili kupata nafasi  hizo za ajira ni mara nyingi uwa ni kuanzia ngazi ya cheti hadi Uzamivu ambapo kuna zaidi ya aina 4000 ya ajira zinazopatikana ikiwamo  Afya,Mauzo,  Masoko, pamoja na  Elimu,”anasema.

Anasema katika kuboresha tovuti hiyo na kuifanya  kuwa na tija kwa kila mwananchi anadai kwamba wapo mbioni kutafuta namna ya kuunganisha katika ajira watu wasio na elimu pamoja na  wanaofanya kazi kutumia nguvu zaidi.

Anasema tuvuti hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo na wafanya kazi wanaotafuta sehemu za kazi zenye maslahi zaidi pamoja na mazingira bora na kudai kwamba si kampuni ya kitapeli kwa kuwa inaaminika na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles