Fundi viatu kizimbani kwa Mauaji

0
636

ERICK MUGISHA-DAR ES SALAAM 

Fundi viatu ambaye ni mkazi wa Buguruni Madenge, Ramadhani Saidi (40), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kuua kwa kukusidia.

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Hilda Katu akimsomea hati ya mashataka mbele ya Hakimu Hudi Hudi alidai Julai 1 mwaka huu Akiwa Mataa ya Mbuyuni Wilayani Kinondoni,  Dar es salaam alimuua Leonce Mapunda kwa kukusudia. 

“Upelelezi wa shauri hili hauja kamilika na tunaomba mahakama kutoa tarehe nyingine kwa kutajwa na kukamilisha upelelezi”, alidai Katu. 

Hakimu Hudi alisema mshtakiwa hataruhusiwa kujibu chochote hadi upelelezi wa kesi hiyo kukamilika na kuhamia mahakama kuu kuendeshwa na jaji. 

“Mshtakiwa utakuwa ukitokea rumande hadi mwisho wa kesi kwa muujibu wa sheria na kanuni la kosa hautakuwa na dhamana,  kesi itatajwa tena Novemba 11 mwaka huu. 

Wakati huo huo Mkazi wa Madale , Abubakary Mselemu (30) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la Kuua kwa kukusudia. 

Mwendesha Mashtaka wa Serikali,  Ellen Masulali akimsomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Happiness Kikoga alidai January 2 mwaka huu akiwa Mbopo center wilayani Kinondoni,  Dar es salaam alimuua Rose Chalse kwa kukisudia .

“Upelelezi wa shauri hili hauja kamilika na tunaomba mahakama kutoa tarehe nyingine kwa kutajwa na kukamilisha upelelezi “,alidai Masulali.

Hakimu kikoga alisema mshtakiwa hataruhusiwa kujibu chochote hadi upelelezi wa shauri hilo kukamilika na kuhamia mahakama kuu kuendeshwa na jaji.

“Mshtakiwa utakuwa ukitokea rumande hadi mwisho wa kesi kwa muujibu wa sheria na kanuni la kosa hautakuwa na dhamana, kesi itatajwa tena Novemba 7 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here