25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

FULANA ZA ‘PRAY FOR LISSU’ HAZIJAZUIWA – POLISI

Na JOHANES RESPICHIUS -DAR ES SALAAM

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Lazaro Mambosasa, amekana kuwakamata watu wanaovaa fulana zenye maandishi ya ‘Pray For Lissu’ na kwamba watu waliokamatwa juzi ni wale waliohisiwa kutaka kuandamana isivyo halali.

Akizungumza na MTAZANIA kwa simu jana, Kamishna Mambosasa, alisema wakati askari wakifanya operesheni ya kuzuia maandamano, walipita katika Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na watu walipoiona gari la polisi, walianza kukimbia.

“Askari baada ya kuona watu wameanza kukimbia, waliamua kuwakimbiza kwani walihisi lengo lao lilikuwa ni kuandamana, hivyo waliwakamata vijana watatu na mpaka ninavyoongea leo (jana) tayari wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kila mara kituoni.

“Jeshi la Polisi halijamkamata mtu kwa kuvaa ‘T-shirt’ (fulana) hizo, bali lilikuwa linakamata watu ambao nia yao ilikuwa ni kuandamana siku ya Jumapili… yaani hapo hata kama ungelikutwa umevaa dera au kanzu unataka kuandamana ungelikamatwa,” alisema Kamishna Mambosasa.

Kuhusu tuhuma kwamba polisi walivamia na kuchukua  baadhi ya vifaa vya Chadema katika maduka yaliyopo karibu na ofisi za chama hicho, Kamishna Mambosasa alisema madai hayo hayana ukweli wowote.

Septemba 17, mwaka huu baadhi ya wafuasi wa Chadema na viongozi wa dini, walipanga kufanya maombi kumwombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyelazwa jijini Nairobi nchini Kenya akitibiwa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilipiga marufuku maombi hayo likidai mkusanyiko huo unaweza kuhatarisha amani na kuwataka waandaaji kufanya maombi hayo makanisani na misikitini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles