27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Froome atwaa tuzo nyingine Ubelgiji

Chris Froome
Chris Froome

CITY OF BRUSSELS, UBELGIJI

BAADA ya kutwaa ubingwa wa michuano ya baiskeli ya Tour de France nchini Ufaransa, Chris Froome, ametwaa tena ubingwa Natourcriterium Aalst nchini Ubelgiji.

Ushindi huo ameupata kabla ya saa 24, tangu achukue ubingwa wa Tour de France na kumfanya awe na mataji matatu katika ndani ya miaka minne.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba nyota huyo na timu yake ya Sky, walifika nchini Ubelgiji huku wakiwa wamechelewa lakini hawakuonekana kuwa na wasiwasi na mashindano hayo.

Inadaiwa kwamba katika michuano hiyo mwaka jana, Froome alishindwa kutamba mbele ya mpinzani wake ambaye alijulikana kwa jina la King Peter Sagan.

Baada ya Froome kutwaa taji hilo, alipewa zawadi ya pombe ya kienyeji tofauti na miaka ya nyuma ambapo mshindi alikuwa anapewa shampeni.

Froome amekuwa na furaha kubwa kuongeza idadi ya tuzo msimu huu na amedai ataendelea kufanya hivyo katika michuano mbalimbali.

“Ninaamini nilikuwa na maandalizi mazuri katika michuano ya Tour de France na ndio maana nilifanikiwa kutwaa ubingwa.

“Maandalizi hayo yamenifanya nije kuwa bingwa tena kwenye michuano hii ya Natourcriterium Aalst, sikuwa na uhakika kama ningeweza kufanya hivi kwa kuwa nilikuwa nimetoka kwenye mashindano makubwa.

“Lakini ninashukuru Mungu nimeweza kufanikiwa kutwaa ubingwa huo, nimepata changamoto kubwa kwa kuwa wapinzani wangu walikuwa na ushindani wa hali ya juu,” alisema Froome.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles