23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Friends of Tulia Trust yaaga mashindano

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kampuni ya Michezo ya kubashiri Tanzania Betika katika muendelezo wa sodo 4 Climate, ilicheza mechi kati ya Friends of Tulia Trust na Espanyol ambapo mechi hizo zilichezwa kwa upande wa sodo wanaume na sodo wanawake.

Katika sodo wanawake friends of tulia 1-2 Espanyol na sodo wanaume friends of tulia trust 0-2 Espanyol.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 26, 2023 jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Betika, Tumaini Maligana amesema Friends of Tulia Trust tayari wameaga mashindano.

“Mechi ya Friends of Tulia Trust na Espanyol zilichezwa kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo friends of tulia trust tayari wameaga mashindano,” amesema Maligana.
Aidha ameongeza kuwa mechi kati ya Timu ya Mkuu wa Mkoa (RC FC) dhidi ya Bodaboda wa Msasani FC inatarajiwa kuchezwa Machi 4,2023.

Katika sodo 4 climate itachezeka ligi katika soka la ufukweni wa Coco Beach ambapo Betika wamealika jumla ya timu 8 zitakazoshiriki na ligi hii itaenda kwa muda wa takribani wiki saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles