French Montana: Khloe bado rafiki yangu

0
630

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Karim Kharbouch maarufu kwa jina la French Montana, amesisitiza kuwa, bado ni marafiki na mpenzi wake wa zamani Khloe Kardashian.

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano mwaka 2014 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya mrembo huyo kuachana na mpenzi wake Lamar Odom, lakini uhusiano wake na French Montana ulidumu kwa miezi mitano.

French Montana amesema, kuachana kwao hakukua kwa ugomvi, hivyo walibaki kuwa marafiki na urafiki wao ni mkubwa sana kwa kuwa hakuna ambaye alikuwa na kinyongo na mwenzake.

“Ninaamini uhusiano wetu ulikuwa wa kweli, hapakuwa na tatizo lolote kati yetu, hakuna ambaye alimfanyia kibaya mwenzake na kusababisha kati yetu tushindwe kuwa pamoja kwa namna yoyote,” alisema Montana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here