26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Francine, Rachael Ekyemba toka Canada watoa ‘Siri’

Toronto, Canada

Waimbaji mahiri wa injili kutoka nchini Canada, Francine Ekyemba na Rachel Ekyemba, wamerudi kivingine na wimbo, Siri unaopatikana kwenye chaneli yao ya YouTube ya FRANCINE RACHEL.

Wawili hao ambao ni ndugu wa kuzaliwa kwa baba na mama mmoja ni wazaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) kwenye familia ya kikristo ya watoto tisa na walianza kumtumikia Mungu kwa kuimba katika kanisa Catholic, Congo.

Miaka 10 iliyopita wawili hao walitoa albamu yao ya kwanza inayoitwa Mungu kupita yote yenye jumla ya nyimbo saba na hapo ndipo walipoanza safari ya kutoka Afrika kwenda Canada.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Francine, amesema mambo mengi yalijitokeza na kufanya albamu hiyo isiwafikie watu wengi ila kwa sasa wamerudi kwa mtindo mpya wakiweka tumaini kwa Mungu ambaye ni muweza wa yote ili kusukuma muziki wao na kufika duniani kote.

“Tunayo hamu, shauku, wito na kiu ya kumtumikia Mungu katika ukweli na haki. Kwasasa tumeachia wimbo mmoja unaoitwa Siri au Siri ya Mafanikio ambao ni ushuhuda kuwa mahali tumefika leo ni kwasababu ya huyu Yesu, isingekuwa huruma na neema zake tusingekuwa hapa, pumzi yake ametupa bure bila kulipia kitu,” amesema Francine.

Aidha Rachael, amesema wana nyimbo nyimbo zipo kwenye chaneli yao ya YouTube pia kuna nyingine mpya zitakuja hivi karibuni hivyo mashabiki wakae mkao wa kubarikiwa na mafundisho wanayotoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles