24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

FOUNTAIN GATE WAREJEA KUTOKA CHINA

Na Mwandishi Wetu


WANAFUNZI 12 wa Shule ya Fountain Gate Academy ya Tabata, jiji Dar es Salaam, waliokwenda nchini China kuonyesha tamaduni mbalimbali za Afrika wamerejea.

Wanafunzi hao walipokelewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na wanafunzi wenzao, walimu na baadhi ya wazazi.

Mkuu wa shule hiyo, Japhet Makau, aliliambia MTANZANIA jana kuwa, wanafunzi hao waliungana na wenzao wa nchi zaidi ya 40 duniani.

Alisema tamasha hilo la kila mwaka linafahamika kama tamasha la kimataifa la utamaduni la watoto.

Alisema wanafunzi hao walikuwa nchini China kwa siku 14, wakionyesha tamaduni mbalimbali za Kiafrika kama ngoma, muziki, chakula na mavazi.

Alisema wanafunzi hao walichaguliwa kutoka klabu mbalimbali za wanafunzi wa shule hiyo ambazo hufanya shughuli zake za maonyesho kila Ijumaa.

“Hii ni mara ya kwanza na shule yetu ni pekee iliyopata fursa hii kwa Tanzania, lakini tutakwenda kila mwaka kwasababu ni sehemu ya kuibua vipaji vya wanafunzi,” alisema.

Aliongeza kuwa, wameanzisha klabu nyingi, zikiwamo za muziki, soka, kuogelea na mpira wa mikono, ili kukuza vipaji vya wanafunzi.

“Pia tumeanzisha klabu ambayo wanafunzi wanajifunza masuala ya fedha, kama kutunza akiba na kufanya uwekezaji, ili wakiwa wakubwa iwasaidie na tumeona mwitikio umekuwa mzuri sana,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles