Fomu za uongozi TOC leo

0
633

filbert-bayiNa WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM

FOMU za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), zinaanza kutolewa leo kwenye ofisi za kamati hiyo jijini Dar es Salaam na Zanzibar.

Uchaguzi wa TOC, umepangwa kufanyika Desemba 10 mwaka huu mjini Dodoma, ikiwa ni hatua ya kamati hiyo kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli, kuufanya mji huo kuwa makao makuu ya Serikali.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alisema ni vema wadau mbalimbali wakajitokeza kwa wingi kuchukua fomu.

“Nafasi zitakazogombewa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Mweka Hazina Msaidizi ambapo fomu zake ni shilingi 200,000, wakati watakaojitokeza kuwania nafasi za wajumbe watalipia shilingi 150,000,” alisema Bayi.

Bayi alisema uchaguzi huo utafanyika kwa mujibu wa katiba ya TOC, Ibara ya 20, ambapo mwisho wa kurejesha fomu hizo ni Novemba 15.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here