26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

FMJ kufanya mnada kupitia mtandao

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Meneja mauzo wa Kampuni ya Uuzaji wa vifaa vya Ujenzi FMJ Hardwer Limited Fredrick Sanga amesema kuwa kampuni hiyo inatarajia kufanya mnada wa hadhara kwa njia ya mtandao kupitia vyombo mbalimbali vya habari Agousti 31 mwaka huu.

Sanga amesema kuwa kampuni hiyo haina wasiwasi kutokana na uchaguzi ujao hivyo kuendelea kufanya mnada kwa njia ya mtandao kutokana uwepo wa amani na utulivu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alisema Kampuni hiyo inaendelea kuunga mkono azma ya Rais wa Tanzania Dk John Magufuli katika ujenzi ya Tanzania ya viwanda.

“Kwa kuunga mkono kasi ya Rais Magufuli kwa vitendo na si kwa nadharia tunatarajia kufanya mnada wa awamu ya pili ujulikanao kama ‘Njoo Upate Bei yako’ mbaya huo utafanyika mwezi Agosti 31 kupitia mtandaoni.

“Vifaa vitakavyouzwa ni vifaa vyote vitakavyotumika kwenye ujenzi wa nyumba ,ofisi, shule na majengo kuazia hatua ya awali hadi kumaliza nyumba kama mabati,nondo,misumari na zingine ,,”amesema.

Ameeleza kuwa lengo ni urahisi wa kumfikia mwananchi popote pale alipo kupitia vyombo vya habari na ili kumwezesha mwananchi kumiliki nyumba bora.

“Kama mtu anataka kufanya manunuzi awasilian kwa namba 0653312438 na 0716902995 pia tunapatikana kwa njia ya WhatsApp, Instagram na facebook kwa jina la Fmj Hardwer lakini unaweza kufika Buguruni Kisiwani,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles