29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, September 18, 2021

FMJ kufanya mnada kipindi cha kampeni

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Uuzaji wa vifaa vya Ujenzi ya FMJ Hardwer Limited, Fredrick Sanga amesema kuwa kampuni hiyo haina wasiwasi kutokana na uchaguzi ujao hivyo kuendelea kufanya mnada kwa njia ya mtandao kutokana uwepo wa amani na utulivu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari amesema Kampuni hiyo inaendelea kuunga mkono azma ya Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli katika ujenzi ya Tanzania ya viwanda.

“Kwa kuunga mkono kasi ya Rais Magufuli kwa vitendo na si kwa nadharia tunatarajia kufanya mnada wa awamu ya pili ujulikanao kama ‘Njoo upate bei yako’ utakaofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia mtandaoni.

“Vifaa vitakavyouzwa ni vifaa vyote vitakavyotumika kwenye ujenzi wa nyumba, ofisi, shule na majengo kuazia hatua ya awali hadi kumaliza nyumba,”amesema.

Ameeleza kuwa lengo ni urahisi wa kumfikia mwananchi popote pale alipo kupitia vyombo vya habari na ili kumwezesha mwananchi kumiliki nyumba bora.

“Kama mtu anataka kufanya manunuzi awasiliane kwa namba 0653312438 au 0716902995 pia tunapatikana kwa njia ya WhatsApp, Instagram na facebook kwa jina la Fmj Hardwer lakini unaweza kufika Buguruni Kisiwani,”amesema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,718FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles