28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

FM Academia kukiwasha, yawaita wapenzi wa burudani Brake Point Dar

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

Unaikumbuka FM ACADEMIA ‘Wazee wa Ngwasuma’ kama uliwahi kuwasikia na hukubahatika kuwaona basi kaa mkao wa kula kwani wanarudi.

Nguli wa Muziki wa Dansi nchi, Nyoshi El Saadat amewataka wapenzi wa muziki huo kujitokeza kwa wingi katika tamasha la kusherekea miaka 62 ya Uhuru wa Demokrasia ya Kongo ambao utaongozwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Julai 2, katika ukumbi wa Brake Point, Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Rais wa FM Academia, Nyoshi El Saadat akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.

Ikumbukwe kuwa bendi hiyo ambayo mwaka 1997 chini ya Rais wake Nyoshi sambamba na Patcho Mwamba ‘Tajiri’, Jose Mara, Kitokololo na wengine wengi, ilijizolea umaarufu kupitia tunzi mbalimbali zikiwamo Duniania Kigeugeu, Malkia wangu, Kizingimngara, Heshima kwa Wanawake na vingine vingi kabla ya kusambaratika

Akizungumza Dar es Salaam leo Alhamisi Juni 30, 2022 Nyoshi amesema siku hiyo kutakuwa na wanamuziki na wanenguaji wote ambao waliwahi kuimba katika bendi hiyo wakisindikizwa na Twanga Pepeta pamoja na Tukuyu Band.

“Niwakaribisha wadau na mashabiki wa muziki wa dansi katika onyesho hili maalum ambalo litatukutanisha wasanii wote waliowahi kutumbwiza ndani ya FM Academia, hii ni wiki ya tatu tupo kambini kwa ajili ya kujifua,” amesema Nyoshi.

Nae, Luiza Mbutu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Dansi (CHAMUDATA), amesema onyesho hilo ni mwanzo wa kuirudisha bendi hiyo ambayo ilijizolea mashabiki wengi na kuwapongeza wasanii hao kwa kumaliza tofauti zao.

Kwa upande wake Rais wa Twanaga Pepeta, Charles Baba ‘Kingunge’ amewahakikishia mashabiki ushiriki wao katika onyesho hilo na kuahidi kutoa burudani ya kiwango cha juu.

Wasanii wengine watakaotoa burudani siku hiyo ni Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’, Kalala Junior, Msafiri Diof na Papii Kocha.

Kwa mujibu wa Nyoshi, kiingilio katika tamasha hilo kwa Meza ni Sh 500,000 na Kawaida Sh 20,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles