30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Fisi wafukua makaburi  

Na Kadama Malunde, Shinyanga

MABAKI ya miili ya binadamu yameokotwa katika Mtaa wa Butengwa, Kata ya Ndembezi mkoani Shinyanga, baada ya makaburi ya watu wasiokuwa na ndugu kufukuliwa na fisi.

Tukio hilo ambalo limevuta hisia za wananchi wengi, limetokea jana saa moja asubuhi, baada ya wananchi waliokuwa wakienda kwenye shughuli zao kukuta mabaki hayo ikiwamo mifupa yakiwa yamefunikwa na mifuko ya sandarusi katika makaburi mawili yanayodaiwa kuwa na urefu wa futi moja.

Akizungumza na MTANZANIA, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Butengwa, Peter Joseph alisema alipewa taarifa kuwapo mabaki hayo na wasamaria wema.

“Nikiwa na wananchi wa mtaa wangu, tulishuhudia kipande cha mkono wa binadamu kikiwa kimeliwa vidole, nikalazimika kuwasiliana na polisi.

“Baada ya hapo, tulienda eneo la tukio kujionea hali halisi, tulikuta mbwa wengi wakiwa juu ya makaburi wakila viungo vya binadamu, huku makaburi yakiwa wazi,” alisema.

Joseph alisema wiki iliyopita magari ya Serikali ya Manispaa ya Shinyanga yalionekana eneo hilo na inadaiwa yalikuwa na miili ya watu waliofariki dunia na kukaa muda mrefu bila kutambuliwa na ndugu zao.

Alisema mara nyingi inapotokea hali hiyo, uongozi wa manispaa huchukua uamuzi wa kuwazika haraka haraka na kondoka.

Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mageuzi, Mhoja Pius alisema tukio hilo linatokana na uzembe wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutosimamia vizuri mazishi ya watu wasiokuwa na ndugu.

“Haiwezekani kaburi la binadamu liwe na urefu wa futi moja, alafu ndani ya kaburi moja wanazikwa watu zaidi ya mmoja.

“Mara nyingi manispaa wanapokuja kuzika huwa hawatoi taarifa kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa, hili tukio la miili ya binadamu kufukuliwa ni la pili, jingine lilitokea mwaka 2012, tulikuta mtu kazikwa huku mkono ukiwa nje ya kaburi, tukashirikiana na wananchi kufunika kaburi,” aliongeza Pius.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Mika Nyange alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo walifika na kubaini makaburi hayo yalifukuliwa na fisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles