26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Filikunjombe: Ziwa Nyasa lipo salama

Deo-FilikunjombeNa Mwandishi Wetu, Ludewa
MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), amewataka wananchi wanaoishi mwambao wa Ziwa Nyasa kufanya shughuli zao, kwani mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Tanzania na Malawi yanakwenda vizuri.
Kauli ya mbunge huyo imekuja huku nchi hizo zikiwa zimefikishana mbele ya jopo la viongozi wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Msumbuji, Joachim Chisano.
Hayo aliyasema juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kilondo, wilayani hapa, ambapo alisema ameshirikishwa katika mazungumzo kwa muda wote wa mzozo huo lakini bado Rais Jakaya Kikwete amekuwa akihimiza amani miongoni mwa nchi hizo mbili.
“Ninachotaka kuwaambia hapa fanyeni shughuli zetu kwa salama na amani, mazongumzo yanaendelea na yanashirikisha pande zote mbili, nami kama mbunge wenu nimeshiriki mara mbili nikiwa na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba.
“Hakuna wa kuwatisha na ni wazi muda wote Rais Kikwete anataka mazungumzo yaishe kwa njia ya amani na itakuwa hivyo,” alisema Filikunjombe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Juma Madaha alisema kuwa ni lazima wananchi wawe huru kufanya mambo yao hasa shughuli za maendeleo bila vitisho.
“Mimi Mkuu wenu wa wilaya ninafanya kazi usiku na mchana fanyeni shughuli zenu za uzalishaji na hakuna wa kuwatisha na mwambao wa Ziwa Nyasa upo shwari wakati wote.
“Kwa hali hiyo ninawahimiza ndugu zangu vueni kwa amani ndani ya Ziwa Nyasa lakini pia tukumbuke kusomesha watoto wetu pamoja na kujenga maabara ya kisasa ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles