23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Filamu ya Salamu kuzinduliwa Machi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Uzinduzi wa Filamu ya Salamu iliyowashirikisha waigizaji Irene Uwoya, Stephen Almasi, Cojack Chilo maarufu Shaka Zulu na wengine wengi unatarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 3, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Filamu hiyo inayoelezea stori ya watoto wadogo wanaotumika kama chambo katika kufanya uhalifu wa mazao na mifugo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 25, mwandishi na muongozaji wa filamu hiyo Salum Majagi amesema watoto waliocheza humo wanawawakilisha watoto wengine wanaofanyishwa kazi na watu wazima ili kujipatia kipato.

“Tanzania ni moja ya nchi ambazo watoto wanatumikishwa sana hivyo sisi kama wasanii tumeona tutumie sanaa kuikumbusha jamii kuhusu tabia hizi na ndiyo maana tumekuja na filamu ya Salamu,” amesema.

Majagi ambaye pia ndiyo muongozaji wa filamu ya Siyabonga iliyoshinda kama Filamu Bora na Filamu yenye maudhui ya kitaifa katika Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu (SZIFF) zilizofanya jijini Dar es Salaam Juzi Jumamosi Februari 23, amesema katika uzinduzi huo yatakuwepo makampuni mbalimbali ya kimataifa hivyo amewasihi washabiki wa filamu kufika kwa wingi.

Aidha amesema tiketi zitapatikana kwa bei ya Sh 10,000 kawaida na 20,000 VIP na uzinduzi utafanyika City Mall jijini hapa.

Naye mmoja wa waigizaji wa filamu hiyo Cojack Chilo, amesema katika filamu hiyo wamezingatia kila kitu ili kuongeza ubora kuanzia stori, ubora wa picha na mazingira hivyo amewasihi Watanzania kufika siku hiyo na kushuhudia uzinduzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles