28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Fikra za mkewe zilimkimbiza Kibonde,kuzikwa leo

Na GRACE SHITUNDU, DAR ES SALAAM

MTANGAZAJI wa Redio Clouds FM, Gadner G Habash, amesema marehemu Ephraim Kibonde alikuwa akimkumbuka mke wake, Sara, mara kwa mara.

Gadner ambaye ni rafiki mkubwa wa Kibonde, alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds.

Alisema mara nyingi Kibonde alikuwa akitaja mkewe aliyefariki Julai 10, mwaka jana katika Hospitali ya Hindu Mandali.

AliSEMA mkewe alipofariki alianza kupata tabu katika nyumba ile waliyokuwa wanaishi kwa sababu walikuwa pamoja kuanzia uchumba hadi kuwa katika ndoa kwa muda wa miaka 20.

“Baada ya mkewe kufariki nyumba waliyokuwa wakikaa ilikuwa ikimuumiza, ilikuwa inampa kumbukumbu,” alisema.

Gadner alisema katika mazingira ya nyumba hiyo alikuwa anamuona yule mama saa zote na kuna wakati anakupigia simu saa tisa usiku kwamba anashindwa kulala.

Pia alisema hali ile ilikuwa inamsumbua hata ikawa inashusha uwezo wake wakati mwingine.

“Kutokana na hali hiyo ndiyo tukamwambia inabidi uhame ile nyumba, na uache kila kitu, sasa ndiyo wakahamia Mbezi.

“Nilikuwa nikikaa na Kibonde huwa haipiti siku bila kumtaja mkewe na ndiyo ikafanya nigundue kuwa bado ana mawazo ya mkewe na nilikuwa nashiriki katika furaha yake na hata majonzi yake nikawa nashiriki baada ya kugundua hilo.

“Tulivyokuwa msibani kwa Boss Ruge, nilimwambia PeterMo kuwa jukumu analolifanya Kibonde (Mc) linaweza kumrudisha kwenye mawazo na majonzi ya mkewe maana ni miezi nane tu toka mkewe atangulie mbele za haki, lakini nikaambiwa kuwa yeye mwenyewe Kibonde alisisitiza kufanya mwenyewe,” alisema.

Gadner alisema Kibonde alikuwa anapenda familia yake na pia kazi yake.

Alisema Kibonde hakuwai kusumbuliwa na presha bali aanaamini kwamba amefariki kwa ajili ya simanzi.

“Kibonde hakuwa na presha, mnaponiambia leo kapata presha na imemuua nashindwa kuelewa.

“Bado siamini Kibonde amefariki kwa kuugua bali naamini ameugua kwa sababu ya simanzi, sijawahi kumuoana kaumwa kalazwa, tatizo la gesi ni jambo linalomkuta akichelewa kula na huwa analitatua kwa kunywa soda water au kidonge cha kutoa gesi ikaisha,” alisema Gadner.

Pia alisema bado anajiuliza kama ataweza kufanya kipindi bila Kibonde.

Alisema amefanya kazi na marehemu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 15 na walikuwa na muunganiko mzuri uliosababisha vipindi vingine kuanzisha kwa mfumo wa kuwa na timu ya watu wawili.

“Tulikuwa tuna chemistry nzuri, tulikuwa tunafanana namna tunavyofanya kazi na namna tulivyokuwa tunaishi na  tunavyo starehe.

“Kibonde alikuwa ni mtu wa furaha, sijawahi kuona kuwa hana furaha au amekasirika,” alisema. 

Kibonde anatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam na alifariki Machi 7, mwaka huu jijini Mwanza  baada ya kuugua ghafla akiwa katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba.

Pia kwa mujibu baba mzazi wa marehemu, Samson Kibonde, alisema atazikwa leo mahali ambako mkwewe Sara alizikwa.

Viongozi mbalimbali walifika nyumbani kwa kina Kibonde Mbezi Africana kwa ajili ya kuhani msiba huo wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa.

Viongozi wengine waliofika msibani hapo ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Januari Makamba na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

Katika hatua nyingine, Majaliwa, alisema kifo cha Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipokwenda kuhani msiba huo kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu.

“Msiba huu umetushtua sana, na ni tukio ambalo hatukulitarajia ila ni mapenzi ya Mungu. Hivi karibuni sote tulimshuhudia akiongoza ratiba ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na alienda hadi Kagera kumzika,” alisema.

Pia alisema enzi za uhai wake, Kibonde aliyefariki dunia juzi alfajiri jijini Mwanza enzi za uhai wake, alishirikiana vizuri na Serikali katika shughuli mbalimbali na amewaomba wananchi waendelee kushikamana na kuifariji familia. “Tumuombee marehemu apumzike kwa amani,” alisema.

Pia alitoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles