27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Figisu zamng’atua Sumaye Chadema, adai kufedheheshwa

Asha Bani, Dar es salaam


Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amejitoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kulinda usalama wake.

Licha ya hatua hiyo ya kujiondoa, Sumaye amesema hatajiunga na chama kingine cha siasa lakini yuko tayari kusaidia chama chochote kwa kuwapa usahauri iwapo watahitaji.


Amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kufanyiwa figisu na viongozi wa juu wa chama hicho baada ya yeye kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho taifa.


Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 4, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Kwa kitendo hiki kilichotengenezwa na kuongozwa na baadhi ya viongozi wa juu wa chama changu Chadema nimefedheheka sana hasa nikijua eti kwasababu nimekosa adabu kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti taifa.


“Jambo hili limeamsha tena hasira zilizokuwa zimetulia dhidi yangu kutoka kwa marafiki zangu na hasa familia yangu, ningeweza kukaza shingo kama mwanzo na labda yangepita tu lakini malengo yetu tungeyafikiaje kwa demokrasia ndani ya chama.


“Baada ya kutafakari kwa kina ustaarabu unasema Sumaye toka sasa maana hautakiwi, akuchukiaye hakwambii toka bali utaona matendo yake, ninajua wapo watakaosikitika sana lakini wapo watakaofurahi kwasababu ninaondoa msongamano na ushindani hasa katika nafasi ya uenyekiti wa taifa.


“Kwa hiyo nimelazimika kwa kulazimishwa kujiondoa Chadema kuanzia leo hii, kwa tafsiri hii mimi si mwanachama wa Chadema kuanzia sasa na sijiungi na chama chochote cha siasa bali niko tayari kutumika na chama chochote kutoa ushauri,” amesema Sumaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles