28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Fifa kumpeleka Neymar Barcelona

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA wanataka kutumia moja ya vipengele vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumrejesha klabuni hapo staa raia wa Brazil, Neymar, ambapo watatumia Pauni milioni 15 tu kumng’oa PSG.

Katika sheria za Fifa, kipo kingele namba 17, ambacho kinamruhusu mchezaji kununua sehemu ya mkataba wake uliobaki endapo tu alisaini akiwa na umri chini ya miaka 27, pia ameitumikia timu hiyo kwa walau miaka mitatu.

Kwa kuwa Neymar alitua PSG mwaka 2017, hesabu zinaonesha atatimiza miaka mitatu akiwa na timu hiyo ifikapo Agosti 3, mwaka huu, na hakuna amefikisha umri huo kwa kuwa sasa na miaka 28. 

Endapo kila kitu kitakwenda sawa kama anavyotaka Rais wa Barca, Josep Bartomeu, basi litakuwa pigo kubwa kwa PSG kwani mwaka jana walikataa Pauni milioni 150 na sasa itawalazimu kupokea Pauni milioni 15.

Kuhakikisha mambo hayaharibiki safari hii, tayari Rais Bartomeu ameshaajiri mtu maalumu wa kwenda hatua kwa hatua na Fifa, ikielezwa kuwa ni mwanasheria raia wa Ubelgiji.

Ndoto ya mabosi na mashabiki wa Barca ni kurejea kwa ‘MSN’, ushirikiano wa Lionel Messi, Luis Suarez ulioifanya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuwa tishio barani Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles