Fiesta 2016 kuanzia Mwanza

FiestaNa MWANDISHI WETU

TAMASHA la Fiesta 2016 linatarajiwa kuanzia jijini Mwanza, Agosti 20 chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo.

Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, alisema katika tukio hilo linalojumuisha shughuli za kijamii litakuwa na kauli mbiu ya ‘Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Imoooo’.

Naye Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Sebastian Maganga, alisema tamasha hilo linaloingia mwaka wa 15 litafanyika  mikoa 15 ambayo ni Mwanza, Kahama, Kagera, Musoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here