Feza yaiokoa Dar matokeo kidato cha nne

0
1045
Mvano Cobangoh akiwa amebebwa na wenzake

Asha Bani-Dar es salaam

Shule ya Sekondari ya Feza ya jijini Dar es salaam imeendelea kufanya vizuri baada ya kuingia 10 bora katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana.

Feza ni shule pekee kwa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoingia katika kumi Bora na nyingine zikiwa sita kutoka Mkoa wa Mbeya, mbili za Mwanza na mbili za Dodoma.

Mwanafunzi wa Shule ya Feza boys, Mvano Cobangoh ameshika nafasi ya sita kitaifa na pia nafasi ya tatu katika kundi la wavulana kitaifa.

Akizungumza leo wakati akifurahia ushindi shuleni hapo amesema hakuamini kushika nafasi hiyo licha ya kwamba alikuwa na ndoto za kufanya vizuri katika mtihani wake wa mwisho.

“Baba alifariki lakini siku zote nilipokuwa nae alikua akinisisitiza kusoma kwa bidii na hata kumuheshimu mama pindi yeye atakapofariki kwa kuwa alikuwa na ugonjwa ambao ilikuwa ni lazima atuandae katika masiaha yote ikiwemo elimu,.

“Ninaishukuru shule yangu ya Feza kwa kuendelea kumsaidia mama angu hasa kwa kumpunguzia majukumu mengine na kumfanya afanikishe mimi leo kumaliza kidato cha nne na kufanya vizuri,’’amesema Mvano.

Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Upendo Komba amesema kutokana na uwezo aliokuwa nao mtoto wake aliamini angeweza hata kuwa mwanafunzi bora kitaifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here