20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

FESTO SANGA: JOHN TIBER NI MCHEZAJI WETU HALALI

NA LULU RINGO


Klabu ya Singida United imesema mshambuliaji John  Tiber aliyesajiliwa kutoka klabu ya Ndanda ni mchezaji halali wa klabu hiyo na si tofauti na Ndanda wanavyodai kuwa bado wanamkataba naye.

Tiber aliyekua na mgogoro wa mkataba dhidi ya mwajiri wake wa zamani, timu ya Ndanda baada ya timu hiyo kusema mchezaji huyo anamkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo huku mchezaji huyo akisema alikua na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

Mkurugenzi wa Singida United, Festo sanga amesema mchezaji huyo kwa sasa ni mali ya Singida baada ya kukamilisha usajili rasmi na kutambulika na Shirikisho la Mpira Tanzania kama mchezaji halali wa Singida United.

“Tiber ni mchezaji halali wa Singida awali tulikua na mgogoro na timu ya Ndanda juu ya mchezaji huyo baada ya kuonekana ana mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo lakini kwa sasa ni mali yetu na hata sasa yupo kambini na wachezaji wenzake” alisema Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles