30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

FEMI ONE; MREMBO WA KENYA ANAYEPETA NA ‘UTAWEZANA’

 CHRISTOPHER MSEKENA 

KUTOKA nchini Kenya rapa wa kike, Femi One, amefanikiwa kutikisa chati za muziki ndani na nje ya Afrika Mashariki kupitia ngoma yake, Utawezana aliyomshirikisha mkongwe, Mejja. 

Ngoma hiyo imeweza kupenya kwenye mitandao pendwa kama Instagram, Facebook, TikTok, Snapchat na mengineyo huku watu mbalimbali kufanya mashindano ya kucheza wimbo huo wa majibizano baina ya Femi One na Mejja. 

Mrembo huyo pia ameweza kuingiza wimbo wake kwenye orodha ya video vinazotazamwa zaidi Tanzania kwa kushika namba nne YouTube, jambo ambalo si kawaida msanii wa nje kupata nafasi hiyo. 

FEMI ONE NI NANI? 

Jina lake halisi ni Wanjiku Kimani kutoka kabila la Kikuyu, aliyezaliwa mwaka 1994 huko Kasarani, Nairobi nchini Kenya akiwa mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu kwenye familia yao.

Femi One alimaliza masomo yake ya sekondari katika shule ya Gakarara akiwa bado ana mpango wa kuendelea na masomo ya chuo na amekuwa na historia ya kushiriki mambo mbalimbali ya burudani yaliyompa urahisi wa kuingia kwenye muziki akiwa kama rapa huku akiamini kwamba yeye hakuichagua rap ila rap ilimchagua yeye. 

ALIVYOINGIA KWENYE MUZIKI 

Anasema alianza kufanya rap akiwa na miaka 15 akiwa kwenye kundi maarufu la rap nchini Kenya linaloitwa Wenyeji akiwa na marapa wengine wawili wakike ambao ni Samantha na Mary ambao baadaye waliamua kufanya mambo mengine nje ya muziki 

Uwezo wake wa rap ulimpa michongo mingi ndani na nje ya Kenya ikiwamo tamasha alilolifanya Afrika Kusini lililoitwa Fire One The Mountain likiwa linadhaminiwa na WAPI ambayo nyuma yake kulikuwa na msanii, King Kaka. 

Femi anasema, King Kaka alimuuliza kama anaweza kushiriki kwenye remix ya wimbo Ligi Soo na ngoma ilipofanyika rasmi rapa huyo alijulikana ndani na nje ya Kenya na akawa msanii aliyesainiwa na lebo ya Kaka Empire. 

Anasema ushawishi wa yeye kuingia kwenye muziki huo aliupata kwa wakali kama Zakah na Swaleh wa Wenyeji, Eli Sketch, King Kaka na Talib Kweli. 

ANACHOAMINI 

Femi One anaamini zaidi katika kufuata ndoto zake kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuzitimiza. 

NGOMA ZAKE KABLA YA ‘UTAWEZANA’ 

Kabla ya kutikisa na ngoma yake Utawezana, Femi One amewahi kutoa nyimbo kadhaa zilizomuweka sehemu nzuri 

 kama rapa anayewakilisha vyema Kenya. 

Ngoma hizo ni Good Times, Maumbile, Ligi Soo Remix, Karata, Wasupa, Ndio Kusema, Luku Luku, Pilau Njeri, Jah, Tippy Toe, Makali Wao, Zaga Zaga, Tembe na nyinginezo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles