27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Fedha za Uviko-19 zajenga madarasa 60, Ofisi 27 Tabaora

Na Allan Vicent, Tabora

Halmashauri ya Manispaa Tabora imefanikiwa kujenga jumla ya vyumba vya madarasa 60 na Ofisi 27 katika shule mbalimbali za Sekondari na Msingi kwa gharama ya Sh bilioni 1.2.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Tabora, Dk. Peter Nyanja (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Mstahiki Meya Ramadhani Kapela, Naibu Meya na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Mjini Mohamed Athuman Katete wakiomba dua kabla ya kuanza kikao cha madiwani jana.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Dk. Peter Nyanja alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji miradi ya maendeleo katika kikao maalumu cha Baraza la madiwani.

Amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 walipanga kutumia kiasi cha Sh bililioni 1.8 kutoka katika vyanzo vyao vya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo, lakini nje ya bajeti hiyo serikali ikawaletea kiasi cha Sh bil 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na thamani zake zote.

Alibainisha kuwa hadi kufikia mwezi Desemba 2021, walikuwa wamekusanya Sh mililioni 880.5 tu kutoka katika vyanzo vyao kiasi ambacho kisingeweza kutosheleza ujenzi wa madarasa hayo ndani ya miezi miwili.

‘Tunampongeza sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha za kutosheleza ujenzi wa vyumba vya madarasa 60, ofisi za walimu 27 na madawati ya kutosheleza vyumba vyote’, alisema Dk. Nyanja.

Dk. Nyanja alieleza kuwa ujenzi wa madarasa hayo umepunguza kwa kiasi kikubwa sana uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwepo katika shule mbalimbali hivyo kumaliza tatizo la msongamano wa wanafunzi madarasani.

Aidha aliongeza kuwa ujenzi wa madarasa hayo ya kisasa umeboresha mazingira ya kazi kwa walimu ikiwemo ufundishaji na ujifunzaji, kupunguza umbali wa wanafunzi kufika shuleni, pia utaongeza mahudhurio na kupandisha ufaulu.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Ramadhan Kapela alisema maboresho yaliyofanywa kwenye sekta ya elimu pia yamewezesha kujengwa kwa madarasa 14 na Ofisi 6 kwenye shule shikizi 5 ikiwemo umaliziaji wa maboma.

Aidha, alibainisha kuwa kwa kutumia fedha zao za ndani wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Kakola, Kabila, Mtakuja, Kiloleni, Izenga na Misha ikiwemo kuanzisha ujenzi katika shule za Inala, Masimba, Kanyenye kwa gharama ya sh mil 112.5.

Alipongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuwaletea maendeleo wananchi huku akibainisha kuwa Rais Samia amewaletea zaidi ya asilimia 98 ya bajeti yao ya fedha za maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles