27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Fedha za maendeleo ya wananchi zisitumike kulipana posho- Ummy

Anna Ruhasha, Sengerema

Serikali imeagiaza fedha za maendeleo zinazotengwa kupitia mapato ya ndani Sh milioni 400 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza zielekezwe katika kutatua changamoto za wananchi na siyo kulipana posho za safari.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake katika Halmashauri hiyo na kukuta zaidi ya wanafunzi 2,000 wanakaa chini katika shule ya msingi Bungumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu.

Aidha, katika Taarifa ya Mbunge wa Sengerema, Hamisi Tabasamu imethibiasha kuwepo kwa uhaba wa madawati ambapo zaidi ya wanafunzi 2,000 wanakaa chini na shule hiyo inajumla ya wanafunzi 3,018.

Pia Tabasamu ameongeza kuwa kulingana na wingi wa wanafunzi hao ameiomba serikali kusaidia upatikana wa shule nyingine ili kuondokana na msongamano wa wanafunzi kwenye shule hiyo.

“Waziri shule hii ina wanafunzi wengi wanatoka visiwani kulingana na geographia ya kata hii na mwaka 2010 watoto kumi walipoteza maisha ziwani wakati wakija shuleni, nikuombe unisaidie tujenge shule uko japo wananchi wameisha anza ujenzi na mimi tayari nimetoa tofari na fedha,” amesema Tabasamu.

Kufuatia taarifa hizo, Waziri Ummy ameagiza fedha za mfuko wa ndani za maendeleo kuelekezwa kwenye changamoto za wananchi ambapo amebaini kuwa Halmashauri haikuweka kipaumbele katika kutatua changamoto za madawati shuleni hapo.

Katika kutatua changamoto hizo Ummy amesema kuwa ofisi yake imeashanzisha mpango wa kujenga shule zenye changamoto hizo na kusema kuwa Halmashauri hiyo itafikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles