24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

FEDHA ZA ESCROW ZAMWIBUA SHIBUDA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


MWANASIASA Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda amewataka waliopokea fedha za mgao wa Escrow kuzirejesha.

Vilevile alimwomba Rais Dk.John  Magufuli awasamehe.

Shibuda ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Maswa Magharibi na  kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, alisema dini zote zinasema asamehewe yule ambaye anatubu na kukubali.

Alisema   anaona  Ngeleja anatakiwa asamehewe kwa vile  amefanya kitendo cha kishujaa, kukiri  na kuamua kuzirejesha fedha hizo

Shibuda ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Mbunge wa   Sengerema, William Ngeleja (CCM) kurejesha Sh milioni 40.4 alizopewa na mfanyabiashara, James Rugemalira.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Shibuda alisema kitendo kilifanywa na Ngeleja ni cha kishujaa na anapaswa kusamehewa kwa kuwa ametambua kosa lake mbele ya umma.

‘’Kwa kitendo chake Ngeleja kutubu, tukubali tusiwe na inda na choyo ila wale wengine nao wakubali kuzirejesha fedha na Mheshimiwa Rais awasamehe kama dini zetu zinavyosema, mtu akitubu asamehewe,’’alisema.

Wakati huohuo,  Shibuda amewashambulia wapinzani kwa akidai   wanatakiwa kuwa  na ajenda mpya kwa vile  zilizopo, Rais wa sasa Dk. John Magufuli amekwisha kuzitatua kwa kiwango kikubwa.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imo katika dunia ya mabadiliko ya mila, jadi na utamaduni na kokomesha uzembe.

Alisema ajenda ya vyama vya upinzani kama rushwa, ufisadi  imenyauka na kuvitaka kutafuta sehemu ya kutokea.

“Vyama vya upinzani kwa sasa ajenda yao ni nini? Ni zile zile za wakati ule Mwalimu   Nyerere aliporuhusu vyama vingi.

“Wanasayansi walianza na dawa ya Panadol  lakini leo kuna dawa zaidi ya tatu basi na wapinzani wawe na vikosi kazi vya kubuni tiba mbadala ya kutengua utumishi uliotukuka wa Rais Magufuli,’’ alisema.

Shibuda alisema serikali ya awamu ya tano inafanya vizuri huku akidai Taifa limepata Rais mwenye utumishi wachangamfu na kugusa hisia za jamii.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Napinga kuwasamehe.mnaua wezi wa simu nyinyi wasomi mnateteana haiko hii.wafungwe na wafanye kazi ngumu. Taifisha mali zao ambazo zimetokana na hela za wizi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles