24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘FEDHA ZA BAJETI ZITENGWE KULINGANA NA MAKUSANYO YA KODI’

 

 

Na AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

SERIKALI imetakiwa kutenga fedha za bajeti kwa kufuata uhalisia wa makusanyo wanayoyapata ili kuweza kutekeleza mipango  iliyojiwekea ndani ya muda uliowekwa.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia inayojishughulisha na kilimo, Forum CC, Fazal Issa, baada ya Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba, kuwasilisha bajeti yake ya Sh bilioni 267.86.

Taarifa iliyotolewa jana mjini Dodoma na taasisi hiyo iliiomba Serikali kufanya marejeo katika utaratibu wa utengaji wa fedha za bajeti ili kufuata uhalisia wa makusanyo yake.

"Taarifa zinaonesha kuwa, wastani wa utoaji fedha kwa sekta hizi ni chini ya 60% kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 2011/12 mpaka 2015/16, pia kwa 2016/2017, hadi kufikia Machi 2017, Serikali ilikuwa imetoa asilimia 30.5 tu ya fedha zilizotengwa ambazo hazikuweza kukidhi mahitaji yaliyowekwa,” alisema Fazal.

Alisema katika bajeti hiyo ya maendeleo na vyanzo vyake, ni asilimia 42 ambapo vyanzo vya ndani vilichangia asilimia 26 tu.

Alisema kwa mwaka 2017/2018 bajeti ya kilimo ya mwaka asilimia 52 ya fedha zimetengwa kwa ajili ya maendeleo, ambapo vyanzo vya ndani vinategemewa kuchangia kwa asilimia 40.

Alisema serikali inapaswa kuongeza jitihada na kuweka mikakati mahususi na kabambe ya upataji wa mapato zaidi ili kutekeleza miradi ya maendeleo inayowekwa katika bajeti hiyo.

Alisema kuwapo kwa utengenezaji wa bajeti halisia na utoaji wa fedha za kutosheleza na kwa wakati kutasaidia kuinua wizara hiyo.

Alibainisha katika bajeti hii  msisitizo umewekwa zaidi kwenye vyanzo nje ya vya kodi, ikijumuisha mapato ya Serikali za Mitaa na mauzo ya nje ambavyo havifanyi vizuri kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles