27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

FCC yaeleza changamoto bidhaa bandia nchini

NA OSCAR ASSENGA-TANGA

TUME ya Ushindani nchini (FCC),  imesema tafiti zimebainisha kuwa uhalifu unaohusisha bidhaa bandia ni changamoto kubwa kwani wahalifu wamekuwa wakibuni mbinu za kuzalisha na kusambaza bidhaa bandia kwakutumia teknolojia na mbinu za kisasa.

Hali hiyo inaweza kuwa ni  pamoja na kurudisha nyuma juhudi ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa zinaweza kulifanya soko la nchi kutoaminiwa na wawekezaji wa viwanda.

Vile vile tafiti zimebainisha kuwa wafanyabiashara wa bidhaa bandia biashara ya bidhaa bandia inaharibu sifa ya kampuni lakini pia kuokosesha mapato halali kampuni hizo, inawadhuru walaji na kuikoseaha serikali mapato.

Hayo yalisemwa juzi jijini Tanga na Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia ambaye pia ni Mwakilishi wa FCC, Magdalena Utouh wakati wa semina ya wajasiriamali wenye ulemavu wa kutokusikia (Viziwi).

Alisema tume imekuwa ikipeleka elimu kuhusiana na suala la kudhibiti wa bidhaa bandia kwa wadau mbalimbali.

Alisema hatua hiyo imewezesha wadau hao kulielewa tatizo na kulichukulia kwa uzito stahiki ambapo hivi sasa wanakundi kubwa la wadau katika mapambano ya bidhaa bandia ikiwemo kundi la walemavu.

Alisema Shirika la Afya Duniani limebainisha mwaka 2010 kwamba zaidi ya asilimia 8 ya vifaa tiba ulimwenguni ni bandia juhudi za pamoja zilizoshirikisha mamlaka za kiserikali katika nchi 115 ulimwenguni ikiwemo Tanzania kupitia operesheni iliyofanyika mwaka 2015 iliwezesha kukamatwa kwa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya dola za Marekeni milioni 81 huku biashara za bidhaa bandia 2,400 zikifungwa.

“Bidhaa bandia ni bidhaa zinazotengenezwa kwa mrengo wa kuwadanganya walaji ili wapate ujasiri wa kutoa fedha yao wakiamini ni bidhaa halisi na itakidhi matarajio ya matumizi matokeo ya bidhaa bandia ni mabaya na yanaathari hasi kwa njia mbalimbali,” alisema Magdalena.

Kati ya mwaka 2008 hadi 2015 bidhaa za thamani ya dola za kimarekani bilioni 172 zilikamatwa eneo la dawa na vifaa tiba na kueleza kuwa uwepo wa bidhaa bandia unaweza kurudisha nyuma juhudi za serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Akifungua semina hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella,  alisema licha ya kuipongeza tume hiyo kwa kazi kubwa inayoifanya hasa kuyapa elimu makundi ya watu wenye ulemavu lakini alitaka utaratibu huo kuigwa na taasisi, mashirika na watu wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles