27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

FBI yaja na mapya mshambuliaji wa Ohio

OHIO, MAREKANI

MAOFISA wa uchunguzi nchini Marekani wamesema mtu aliyewauwa kwa kuwapiga risasi watu tisa katika jimbo la Ohio nchini humo amekuwa akijihusisha na itikadi ya ghasia.

Shirika la Upelelezi la FBI lilianzisha uchunguzi wake kuhusiana na nia ya mwanaume huyo aliyekuwa na umri wa miaka 24 na limesema kuna mashaka iwapo shambulizi hilo lilichochewa na ubaguzi wa rangi.

Todd Wickerham, wakala wa FBI huko Cincinnati ametoa kauli hiyo licha ya kuwa sita kati ya watu tisa waliouwawa na mshambuliaji huyo walikuwa weusi.

Shambulizi hilo lilitokea saa chache baada ya shambulizi jingine jimboni Texas katika duka la jumla la Walmat mjini El Paso. Jumla ya watu 31 waliuwawa katika mashambulizi yote mawili yaliyohusisha ufyatuaji wa risasi.

Mshambuliaji wa Ohio aliuawa na Polisi.

Rais Donald Trump ambaye anashutumiwa kuhamasisha chuki kupitia kauli zake kali, jana alizuru miji miwili iliyokumbwa na mashambulizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles