NA FESTO POLEA, ZANZIBAR
MWANAMITINDO maarufu visiwani Zanzibar, Farouk Abdillahi, alionekana kuiogopa tuzo aliyotunukiwa ya kutukuka kutokana na mchango wake wa kukuza fani ya mitindo kwa vijana wengi wa visiwani Zanzibar.
Farouk alianza kwa kushukuru tuzo hiyo kwa kuona umuhimu wake lakini alihofia maneno kwamba wanaopata tuzo hiyo huwa wanafariki dunia baada ya miaka michache mbele baada ya kuipokea.
“Nashukuru kwa tuzo lakini hofu yangu ni kwamba ni kweli kwamba watu wanaopata tuzo hii hufariki baada ya miaka michache,” alisema kwa utani huku alaiki ya watu wakicheka.
“Nilipotajwa nilishtuka kwa hofu ninachouliza kinasemwa kwamba watu wanaopata tuzo hii hufa mapema isije kuwa mmenipa hii kunipunguzia uhai wangu,” aliongeza na kuzua kicheko zaidi kwa wahudhuriaji wa tuzo hizo.
Hata hivyo, uongozi wa ZIFF ulimtoa hofu hiyo wakimweleza kwamba wapo wengi waliopata tuzo hiyo na wanaendelea kuishi kwa miaka mingi.