32.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

Faraja Masinde aibuka kinara tuzo za uandishi wa habari za watoto 2022

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mhariri wa MTANZANIA DIGITAL, Faraja Masinde, ameibuka mshindi wa jumla wa tuzo za uandishi wa habari za watoto (TEFCRA) kwa mwaka 2022 zilizoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania, Ousmane Niang akimkabidhi tuzo na cheti cha ushindi wa jumla kwa Mwandishi Faraja Masinde Kutoka Mtanzania Digital baada ya kushinda tuzo ya jumla kuhusu habari za watoto (TEFCRA) kwa mwaka 2022 zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kwa kushirikiana na UNICEF katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam Desemba 29, 2022.

Tuzo hizo zimetolewa Alhamisi Desemba 29, 2022 katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam ambapo Faraja Masinde kutoka Mtanzania Digital ndiye amepata tuzo ya jumla kati yawanahari 12 waliokuwa wakiwania tuzo hizo.

Masinde alikabidhiwa tuzo hiyo ya mshindi wa jumla ya Umahiri wa Uandishi wa Habari za Watoto Tanzaniana kwa mwaka 2022 na Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania, Ousmane Niang, ambapo iliambatana na Cheti, na fedha taslimu Sh 500,000.

Akizungumzia ushindi huo wa jumla, Masinde amesema kuwa tuzo hizo zitakuwa ni chachu ya kufanya kazi nzuri zinazogusa jamii hususan nyanja ya watoto.

“Kwanza nimeshinda tuzo ya Mwandishi Bora wa Takwimu(Data Journalism Award) 2022 na tuzo nyingine ni ya mshindi wa jumla wa tuzo za uandishi wa habari za watoto 2022(Overall Winner).

“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kushinda tuzo hizi, pia nawashukuru UNICEF na TEF kwa kuandaa kitu hiki. Hii imekuwa ni heshima kwangu kuona kwamba UNICEF na TEF wameona ninastahili kushinda tuzo hii hususan katika eneo la kupinga ndoa za utotoni.

“Hivyo nitaendelea kutumia kalamu yangu kuikumbusha Serikali kwamba ni wakati sasa wakufanya mabadiliko ya sheria ya ndoa ili binti aolewe akiwa tayari ana miaka 18 na kuendelea na siyo chini ya hapo kama ilivyo hivi sasa,” amesema Masinde.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TEF, Salim Saidi Salim(kulia) akifurahia jambo baada ya kumkabidhi tuzo, cheti na fedha taslimu Fraja Masinde wakati wa tuzo hizo.

Awali, wanahabari 12 kutoka katika vyombo mbalimbali walipewa Tuzo ya Umahiri katika Uandishi wa Habari za Watoto nchini Tanzania iliyoambatana na cheti pamoja na fedha taslimu Sh 200,000.

Walioshinda tuzo hizo ni Faraja Masinde(Mtanzania Digital) ambayo hiyo inakuwa ni mara yake ya pili baada ya awali kushinda tuzo hiyo mwaka 2021 katika tuzo zilizofanyika mkoani Morogoro.

Wengine walioshinda ni Dk. Tumaini Msowoya(Mwananchi – Shamba Fm), Marco Maduhu (Nipashe), Aidan Mhando (Chanel Ten) na Anord Kairembo (Radio Kwizera).

Wengine ni Vick Kimaro (Habari Leo), Jurieth Mkireri (Nipashe), Judith Ndibalema (Majira), Shua Ndereka (Mviwata Radio),  Sabina Martine (CHAI FM) ya Rungwe mkoani Mbeya  , Anna Sombida (EATV) na Stansaus Lambet (Dar 24).

Mratibu wa tuzo hizo, Neville Meena amesema huo ni mwendelezo wa kuhakikisha habari za watoto zinaendelea kuandikwa.

Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania, Ousmane Niang akimkabidhi tuzo na cheti cha ushindi wa jumla kwa Mwandishi Faraja Masinde Kutoka Mtanzania Digital baada ya kushinda tuzo ya jumla kuhusu habari za watoto (TEFCRA) kwa mwaka 2022 zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kwa kushirikiana na UNICEF katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam Desemba 29, 2022.

Makamu Mwenyekiti wa TEF, Bakari Machumu aliwataka waandishi kuendelea kuandika habari za watoto.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amewata Wahariri na wanahabari kuingia kwenye vita dhidi ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971.

Afisa habari wa UNICEF, Usia Nkoma(kulia) akikabidhi tuo kwa mwandishi Aidan Mhando kutoka Channel Ten mara baada ya kushinda tuzo kwa upande wa luninga kuhusu habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam Desemba 29,2022.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania, Ousmane Niang akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Deodatus Balile katika tuzo za habari za watoto (TEFCRA)zilizoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na kufanyika leo Kwenye hoteli ya Peacock jijiniDar es Salaam, Desemba 29,2022.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles