24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

Familia yamweka sawa P. Diddy

NEW YORK, MAREKANI

RAPA P. Diddy ameishukuru familia yake kwa kumfanya arudi katika hali ya kawaida tangu alipofiwa na mama wa watoto wake, Kim Porter.

Kim Porter alipoteza maisha Novemba mwaka jana huku akiwa na umri wa miaka 47. Wawili hao katika uhusiano wao walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha ambao ni D’Lila Star na Jessie James wenye umri wa miaka 12.

Kupitia ukurasa wa Instagram, P. Diddy aliposti picha ya mapacha hao wakiwa na marehemu mama yao enzi za uhai wake na kuweka wazi kuwa, watoto hao wamechangia kwa kiasi kikubwa kumweka sawa.

“Baada ya Kim kufariki dunia, ukweli ni kwamba nilikuwa katika wakati mgumu, lakini nashukuru familia yangu imekuwa pamoja na mimi kuhakikisha ninarudi katika hali ya kawaida. Naipenda familia yangu, Mungu nakushukuru kwa kila kitu,” aliandika P. Diddy.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,646FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles