33.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

FAMILIA YAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKEKETA WATOTO

law-portal

Na MALIMA LUBASHA -SERENGETI

FAMILIA ya watu watatu wa Mtaa wa Chamoto, Kata ya Stendi Kuu, Tarafa ya Rogoro wilayani Serengeti mkoani Mara, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili watoto wawili wa kike kwa njia ya ukeketaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Pascal Nkenyenge, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Amaria Mushi, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Ikwabe Charali (32), Robi Petro (31) wakazi wa Chamoto na Nyangi Charali (35) mkazi wa Kijiji cha Matare wilayani hapa.

Alisema washtakiwa hao ambao ni baba, dada na mke wa mshtakiwa wa kwanza Ikwabe, wanatuhumiwa kuwafanyia ukatili watoto wa kike kwa kuwakeketa Desemba 19, mwaka huu ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.

Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka mawili  yanayowakabili  katika kesi hiyo, walikana kuhusika na tukio hilo kwani walitenda kosa hilo.

Hakimu Mushi, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 2, mwakani itakapotajwa tena hivyo kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu.

Wakati huo huo, Mkazi  wa Kijiji cha Bonchugu, Kata ya Manchira wilayani Serengeti mkoani Mara, Chacha Matiko (53), amehukumiwa na mahakama hiyo kifungo cha miaka  mitatu  jela na kulipa faini ya  Sh 800,000 baada ya kupatikana  na makosa  ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kuchunga ng’ombe bila kibali.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile.

Alisema mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles